Mkakati wa uwezeshaji wa wananchi kiuchumi ulioanzishwa na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kuwainua wananchi kiuchumi na kuboresha maisha ya wananchi kwa ujumla, umeonekana kuzaa matunda makubwa katika Mkoa wa Kigoma kwa kuinua pato la uchumi kibiashara na shuguli za ujasiliamali kwa wanaume, wanawake na vijana.
Haya yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brig. Jen. Mstaafu Emanuel Maganga wakati akikabidhiwa kombe na cheti cha ushindi kwa nafasi ya pili Kitaifa Katika kuwezesha wananchi kiuchumi.
Akikabidhi kombe hilo kwa Halmashauri za Mkoa wa Kigoma, Mhe. Maganga ameeleza kuwa juhudi kubwa ambazo zimefanywa na Serikali ya Mkoa wa Kigoma ni kusimamia na kuwawezesha Wananchi kiuchumi ikiwa pamoja na kutoa mikopo, kuwapa elimu na mafunzo ya Ujasiliamali wanachi kupita Mabaraza ya Biashara ya Wilaya.
Naye Afisa wa Dawati la Uwezeshaji Kiuchumi la Mkoa wa Kigoma (RECO) Bw. Deogratias Sangu ameeleza mafanikio ya kushika nafasi ya pili yametokana na kukidhi vigezo Katika utekelezaji wa mambo yote yaliyopangwa kama msingi wa kuinua wananchi kiuchumi.
Sangu ameongeza kuwa, Mwaka jana (2017) Mkoa wa Kigoma ulishika nafasi ya mshindi wa tatu Kitaifa, na kwamba juhuzi kubwa imefanyika katika kuwezesha wananchi na kutekeleza vigezo vilivyowekwa kiushinfdani na kufanikiwa kufikia nafasi ya pili kwa mwaka 2018, ninaamini ushindi huu umetupa hamasa kimko ya kufanya vizuri zaidi ili kushika nafasi ya kwanza aliongeza Bw. Sangu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti wawakilishi wa wananchi kutoka katika vikundi, Asasi na jumuia za wafanyabiashara waeelezea kufurahishwa na juhudi zinazofanywa na Serikali ya Mkoa wa Kigoma katika kuinua uchumi wa wananchi.
Serikali ya Mkoa wa Kigoma imeahidi kuendelea kuwawezesha wananchi katika shughuli za ujasiriamali na uanziashaji wa viwanda vidogo ili kuongeza thamani ya mazao yanayozalishwa Mkoani humo, ili kutoa tija zaidi katika biashar wanazofanya wajasiriamali hao.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa