Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jen.(mst) Emannuel Maganga amemtaka Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Umeme REA III katika Wilaya za Kibondo na Kakonko kuongeza kasi ili wananchi wapate umeme.
Maganga amesema haridhishwi na kasi ya Mkandarasi huyo ambayo inaendelea kuwaweka wananchi gizani licha ya Serikali kumlipa fedha Mkandarasi huyo.
Aidha imeelezwa kuwa Mkandarasi aliahidi mbele ya Naibu Waziri wa Nishati wakati wa uzinduzi wa Mradi huo kuwa angekamilisha mradi huo mwezi Februari 2018, lakini hadi sasa abaendelea kusuasua.
"Sioni sababu ya kutokamilika kwa mradi kwani Serikali imeshatoa pesa kwa Mkandarasi na hana sababu za kuchelewesha mradi, sitavumulia endapo utaonekana ni tatuzi nitakuondoa haraka Mkoani kwangu" alisisitiza Maganga.
Mradi wa Umeme REA III Mkoani Kigoma unatekelewa katika tarafa za Mabamba Wilayani Kibondo na Juhudi Wilayani Kakonko, ulizinduliwa mapema mwezi Februari mwaka huu amabapo Mkandarasi Kampuni ya Rural and Urbarn Engeneering Services aliahidi kuwasha umeme katika maeneo hayo mwishoni mwa mwez Februari.
Naye Mkandarasi wa Kampuni ya Rural and Urban Engeneering ametaja changamoto kadhaa zinazomfanya asikamilishe ikiea pamoja na jiografia ya maeneo na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo hayo. Hata hivyo ametakiw ameahidi kukamilisha mradi mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa