MIKAKATI YA UANZISHWAJI WA BENKI YA WANANCHI MKOANI KIGOMA
Posted on: October 26th, 2017
Mchango wa sekta binafsi kwa kushirikina na serikali ni pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo, chachu kubwa ya maendeleo katika kufanikisha dira ya serikali ya nchi ya viwanda na kufikia uchumi wa kati.
Amesema Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jeerali Maganga wakati wa kikao cha Kikosi kazi kilichoundwa kuratibu zoezi la uazishwaji wa Benki ya Wananchi Mkoani.
Kwa kushirikiana na sekta binafsi Mkoa wa Kigoma umeanza kutekeleza agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alilolitoa Mjini Dodoma kuhakikisha Kila Mkoa uwe na Mkakati wa kuanzisha taasisi za kifedha za wananchi yaani Benki ya Wananchi.
Uanzishwaji wa Benki ya wananchi Mkoani Kigoma unalenga kuchochea maendeleo kiuchumi kwakuwawezesha wananchi kupata huduma za kifedha katika Benki hizo kwa masarti nafuu.
Ni fursa nzuri kwa wajasiriamali na wakulima kuweza kupata mikopo kwa riba nafuu ili kukuza mitaji yao.
Katika kufikia dhamira ya viwanda na nchi ya uchumi wa kati, nilazima kuwepo na mikakati yakuwawezesha wananchi kifedha ili waweze kuwekeza katika viwanda.
Jitihada hizi zitawezekana ikiwa kuna mikakati madhubuti ya uwepo na upatikanaji wa taasisi za kifedha zenye kuwafikia wananchi na kwamasharti nafuu.
Mkuu wa Mkoa amewataka wajumbe wa kikosi kazi kinachoratibu uanzishwaji wa Benki ya wananchi Mkoani Kigoma wafanye kazi kwa moyo na weledi kuwasaidia wananchi na kutimiza dhamira ya serikali kufikia uchumi wa kati na Viwanada.
Mimi nawaambia usipoacha alama yeyote hapa duniani kwa kufanya matendo mema, kujitoa kuwatumikia wengine kuiko kujijali wewe na maslahi yako wewe huwezi kukumbukwa hata kidogo, nawaomba suala hili mlipe kipaumbele kila siku katika mafikirio yenu. Alimalizia Magaga.