Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb) awasili Mkoani Kigoma kufanya Ziara ya Kikazi ya siku Nne (4) kuanzia tarehe 16 hadi 19 Februari, 2019. Akiwa Mkoani Kigoma Waziri Mkuu amepokelewa na Mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Viongozi mbalimbali wa chama na Serikali pamoja Wananchi.
Ziara hii ni mwendelezo wa Ziara yake Mkoani Kigoma aliyoifanya mwaka jana 2018 kwa lengo la kuangalia na kuhamsisha uendelezwaji wa Kilimo cha Zao la Michikichi na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.
Akiwa Mkoan Kigoma Mhe. Waziri Mkuu atakagua vitalau vya uoteshaji wa mbegu za Michikichi na shughuli mbalimbali zinazohusiana na mnyororo wa thamani wa zao la Michikichi pia kuendelea kutoa msisitizo na msukumo kwa wananchi wa Mkoa wa Kigoma ili kufufua na kuendeleza Kilimo cha zao la Michikichi.
Pamoja na kukagua shughuli mbalimbaliza maendeleo Mhe. Waziri Mkuu atapata fursa ya kuzungumza na Wananchi katika maeneo mbalimbali ya Wilaya za Kigoma, Uvinza, Kibondo na Kakonko.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa