MICHEZO YA UJIRANI MWEMA YAENDELEA KURINDIMA MKOANI KIGOMA
Michuano ya Ligi ya Mpira wa miguu Lake Tanganyika Cup imeendelea kurindima katika viwanja vya Uhuru wikayani Kasulu na Lake Tanganyika Manispaa ya Kigoma Ujiji, huku timu mbalimbali za Mkoa wa Kigoma na Kagera zikichuana kuwania kombe litakalo shindaniwa na mshindi kutoka Tanzania na Burundi.
Mashindano ya ligi hiyo kwa sasa yapo katika hatua ya mzunguko na baadaye mtoano wa timu za Kundi A na B. Kundi A ikihusisha timu kutoka Uvinza, Buhigwe, na Kigoma Mjini zinazoendelea kuchuana katika Uwanja wa Lake Tanganyika na zile za kundi B kutoka Wila za Kasulu, Kibondo, Kakonko na Ngara zinaendelea kucheza katika uwanja wa Uhuru uliopo Wilayani Kasulu.
Ligi ya Lake Tanganyika Cup ni matokeo ya makubaliano ya vikao vya kamati za Ulinzi na usalama kati ya Mkoa wa Kigoma na Mikoa ya Nchi jirani ya Burundi inayopakana na Tanzania ambayo ni Ruyigi, Cankuzo,Rutana, Rumonge na Makamba.
Michezo hii inalenga kuleta ushirikiano wa mambo mbalimbali kati ya Burundi na Tanzania ikiwe diplomasia, kujenga urafiki, undugu, mahusiano mema kati ya wananchi wa Mikoa ya Burundi inayopakana na Mkoa wa Kigoma.
Akiongea wakati wa Uzinduzi wa Ligi hiyo kwa Upande wa Tanzania Mkuu wa Mkoa wa Kigoma amezitaka timu zishindane kistaarabu na si kwa kurushiana ngumi na maneno yasiyoendana na maadili ya mchezo wa soka. Aidha amewaomba wananchi wa mkoa wa Kigoma wafike kushuhudia mechi hizo kiingilia ni bei ya kawaida kwa wote.
Kwakuonesha umuhimu wa ligi hiyo Rais wa Chama cha Mpira ambaye pia ni Spika wa Seneti ya Burundi Bw. Reverien Ndikuriyo aliahidi kutoa vifaa vya michezo pamoja na Kombe ambalo litakaloshindaniwa na timu mbalimbali kutoka Burundi na Tanzania. Ligi itahitimishwa kwa fainali kati ya Mshindi mmoja kutoka Mkoa wa Tanzani na Timu kutoka Burundi ambapo atajinyakulia Kombe siku ya tarehe 28 Oktoba, 2017 katika uwanja wa Lake Tanganyika.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa