Jumla ya Miradi 73 yenye thamani ya Shilingi Bil. 21.3 itazinduliwa, kukaguliwa, kuwekewa mawe ya msingi na kutembelewa na mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa Mwaka 2024 Mkoani Kigoma.Kupitia hotuba aliyoitoa wakati wa mapokezi ya mbio hizo, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye amesema miradi 10 itawekewa mawe ya Msingi, mitatu (3) itafunguliwa, 27 itazinduliwa, 24 itatembelewa na kukaguliwa huku miradi 9 ikihusisha ugawaji wa vifaa kwa vijana wajasiriamali na misaada kwenye shule na vituo vya kulea watoto wenye mahitaji maalum.Amesema katika miradi itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru mkoani Kigoma, miradi iliyotekelezwa kwa mchango wa nguvu za wananchi inathamani ya Shilingi 105. Sawa na 0.5%, halmashauri za wilaya zikichangia Shilingi Bil 1.0 sawa na 4.8%, serikali kuu ikichangia Bil.16.9 sawa na 79.1 na michango ya wahisani ikiwa ni Bil.3.3 sawa na 15.6%.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa