Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2024 zimeanza mkoani Kigoma ambapo jumla ya Miradi 73 yenye Thamani ya Shilingi Bil. 21.3 imeanza kutembelewa, kukaguliwa, kuwekewa mawe ya Msingi na kutembelewa na mbio hizo za kitaifa.
Septemba 14,2024 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ameupokea Mwenge huo wilayani Uvinza ukitokea mkoani Katavi ambapo kupitia taarifa aliyoitoa wakati wa mapokezi ya Mwenge hu, Jumla ya Miradi kumi(10) itawekewa Mawe ya Msingi, mitatu(3) itafunguliwa, 27 itazinduliwa, 24 itatembelewa na kukaguliwa huku miradi 19 itahusisha ugawaji wa Vifaa kwa vijana wajasiriamali na misaada kwenye shule na vituo vya kulea watoto wenyemahitaji maalum.
Mhe. Andengenye ameendelea kufafanua kuwa katika miradi hiyo, inayotekelezwwananchi inathamani ya Shilingui Mil 105 sawa na Asilimia 0.5, halmashauri za wilaya ni Bil1.0, sawa na asilimia 4.8, serikali kuu ikichangia Bil. 79.1 ma michango ya wahisani ikifikia Bil.3.3 sawa na 15.6 Asilimia.
Mpaka kufikia Leo Septemba 16,2024 miradi yote iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru imepokelewa na kiongozi wa mbio hizo kitaifa.
Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru zimetembelea miradi mbalimbali katika wilaya za Uvinza, Kigoma na Manispaa ya Kigoma Ujiji ambapo kiongozi huyo wa mbio za Mwenge kitaifa ameonesha kuridhishwa na utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika maeneo hayo.
Akiwa katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, kiongozi huyo ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kutumia fedha zitokanazo na Makusanyo ya Ndani kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ambapo kiasi cha Shilingi 130,000,000 kinatumika katika ujenzi wa zahanati Kitongoni huku kiasi cha Shilingi 57,000,000 kikitumika katika ujenzi wa Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Buhanda.
Akiwa katika wilaya ya Kigoma, kiongozi huyo amefungua mradi wa upanuzi wa Mradi wa Maji Kidahwe ambao umetajwa kuwa mkombozi kwa wakazi wa eneo hilo kwani kukamilika kwake kutafanikisha dhamira ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu ya kumtua mama ndoo kichwani.
Mradi huo unatarajiwa kuwaondolea kero ya ukosefu wa maji wakazi takribani 2000 huku maboresho hayo yaakiongeza upatikanaji wa huduma hiyo hadi kufikia Lita 300,000 kwa siku.
Awali mara baada ya Mwenge huo kuanza mbio zake mkoani hapa, kiongozi huyo wa mbio za Mwenge kitaifa amewataka wakazi wilayani Uvinza na Mkoa wa Kigoma kwa ujumla kujikita katika kilimo cha zao la chikichi kutokana na bidhaa za zao hilo kuwa na uhakika wa masoko ndani nan je ya mkoa wa Kigoma.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa