• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko / Mrejesho |
KIGOMA   REGION
KIGOMA   REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Kigoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Seksheni ya Elimu
      • Seksheni ya Afya
      • Seksheni ya Miundombinu
      • Seksheni ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Mipango na Uratibu
      • Seksheni ya Uchumi na Uzalishaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha Fedha
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwami
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Kibondo
      • Halmashauri ya Kibondo
    • Wilaya ya Kigoma
      • Halmashauri ya Kigoma
      • Manispaa ya Kigoma Ujiji
    • Wilaya ya Kakonko
      • Halmashauri ya Kakonko
    • Wilaya ya Kasulu
      • Halmashauri ya Kasulu
      • Halmashauri ya Kasulu Mji
    • Wilaya ya Uvinza
      • Halmashauri ya Uvinza
    • Wilaya ya Buhigwe
      • Halmashauri ya Buhigwe
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Kigoma Ujiji
    • Halmashauri ya Buhigwe
    • Halmashauri ya Kasulu
    • Halmashauri ya Kasulu Mji
    • Halmashauri ya Kibondo
    • Halmashauri ya Uvinza
    • Halmashauri ya Kakonko
    • Halmashauri ya Kigoma
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Kigoma Special Economic Zone
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mikakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Picha

Matumizi ya Simbomilia (Barcodes) katika bidhaa ni jambo lisilokwepeka Kuelekea Nchi ya Viwanda Tanzania

Posted on: April 11th, 2017

Matumizi ya Simbomilia (Barcodes) au alama za utambuzi wa bidhaa katika masoko ni jambo lisilokwepeka kwa sasa ambapo Tanzania inaelelekea kweye nchi ya uchumi wa kati na viwada. Haya yameelezwa na Mkurugezi wa Taasisi ya Global Standard one (GS1) Tanzania Bi. Fatma Kange Salehe wakati wa kutia saini ya makubaliano na Halmashauri nane za Mkoa wa Kigoma.Mkataba wa Makubaliano na Taasisi ya GS1 Tanzania unalenga kuwapa mafunzo na kuwajengea uwezo wajasiriamali katika Halmashauri ili waweze kutambua umuhimu wa kuwa na alama za utambuzi wa bidhaa katika masoko wanazozizalisha. Mafunzo hayo yanatarajiwa kuzijumuisha Taasisi mbalimbali zitakazoshiriki katika utoaji wa mafuzo hayo kwa wajasiriamali kama vile Wakala la Vipimo, Mamlaka ya Mapato Tazania, Shirika la Viwago Tanzania, BRELLA, SIDO, TANTRADE. Matarajio baada ya mafunzo haya ni, kuongezeka kwa mapato ndani ya Halmashauri, bidhaa nyingi kuwa katika soko rasmi kitaifa na kimataifa, kuongeza mnyororo wa thamani ya bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali, kuongezeka kwa wajasiliamali katika Halmashauri na, kuwanyanyua kiuchumi wajasiliamali wadogo. Naye Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brigedia Jenerali Emanuel Maganga (mst) ambaye alishuhudia utiwaji wa makubaliano hayo kati ya GS1 Tanzania na Halmashauri za Mkoa wa Kigoma alisema kuwa lengo la Serikali ya Mkoa wa Kigoma ni kuhakikisha kwamba fursa zote za kilimo, uvuvi na madini zinafanyiwa kazi kisasa zaidi ili wananchi waweze kumiliki Uchumi. “ili wananchi wetu waweze kunufaika na kilimo, vuvi, madini lazima kuwepo na mbinu sahihi za kuongeza thamani kwenye bidhaa zao wanazozalisha na zikubalike katika masoko ya ndani nje” alisisitiza. “Ninaamini makubaliano haya yatakuwa na matokeo chanya ambayo yatawezesha bidhaa nyingi za Tanzania hususani wananchi wa Kigoma kuingia katika Masoko ya ndani na nje ya nchi hivyo kuinua pato la mtu mmoja mmoja na hatimae taifa zima” aliongeza Maganga. Aidha, amewaasa watanzania kuanza kutumia Simbomilia (barcordes) za Tanzania badala ya kutumia za nje ya nchi. Alisisitiza kuwa kutumia simbomilia za Tanzania kutapunguza matumizi ya fedha za kigeni ambazo zingetumika kulipia uduma hiyo, pia itasaidia kutoa takwimu rasmi za wazalishaji wa Kitanzania, kwani unapotumia simbomilia za nje ya nchi bidhaa huonekana imetoka nchi nyingine na siyo Tanzania hata kama imezalishwa hapa nchini. Kutokana na umuhimu wa jambo hili Maganga amewaagiza Wakurugenzi kuanza mafunzo haya kwa wajasiliamali ndani ya Miezi miwii tangu kutiwa saini ya Makubaliano na Taasisi ya GS1 Tanzania.

Matangazo

  • MAZOEZI KWA AFYA YAKO March 23, 2017
  • UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024 September 12, 2024
  • UJIO WA MADAKTARI BINGWA MKOANI KIGOMA November 12, 2018
  • Fomu ya Usajili wa Maonesho TBS Kigoma May 01, 2022
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • RC ANDENGENYE AKABIDHI VITENGO VITENGO VYA LISHE MKOA NA WILAYA UVINZA

    May 09, 2025
  • DCP NARCIS MISSAMA AFANYA ZIARA MKOANI KIGOMA

    May 07, 2025
  • JAJI ASINA AKAGUA ZOEZI LA UBORESHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI-KIGOMA

    May 03, 2025
  • VYAMA VYA WAFANYAKAZI VISIGEUKE MAHAKAMA ZA KUWAHUKUMU WATUMISHI-RC ANDENGENYE

    May 01, 2025
  • Ona vyote

Video

RC ahimiza wananchi anuani za Makazi
Video nyingine

Tovuti zinazo fanana

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA BUHIGWE
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KAKONKO
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
  • HALMASHAURI YA MJI KASULU
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBONDO
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA
  • HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGOMA UJIJI
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA UVINZA

Tovuti zinazo husiana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI PORTAL
  • IKULU
  • OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    MKOA WA KIGOMA

    Anuani: S.L.P 125

    Simu: 0282802330

    Simu ya kiganjani: +255766853404

    Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://bachelorthesiswritingservice.com

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa