Sekta ya Afya Mkoani Kigoma imeimarika kutokana na Mashirika ya Thamini Uhai, Bloomberg Foundation na Engeder Health kujikita katika kusaidia Mkoa katika sekta ya Afya.
Mashirika hayo yasiyo ya kiserikali yanatarajiwa kukabidhi miradi ikiwemo Miundombinu ya Majengo ya maabara, vifaa tiba, kugharimia posho za watumishi wa Afya wanaojitolea katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kigoma hasa pembezoni.
Wakiongea kwa nyakati tofauti tofati wawkiishi wa mashirika hayo wameuomba Uongozi wa Mkoa kujiandaa kupokea miradi hiyo na kuitunza pamoja na kuiendeleza kwa manufaa ya wananchi wa Kigoma.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ameyapongeza mashirika hayo kwa kuwa na moyo wa dhati katika kuwasaidia wananchi wa Mkoa wa Kigoma katika masuala ya Afya, aidha aliongeza kuwa sekta ya Afya Mkoa wa Kigoma imeimarika, zaidi Mkoani Kigoma kutokana na Serikali kushirikiana kwa karibu na wadau mbalimbali na alisema kwa sasa Mkoa unatarajia wafayakazi wengi zaidi kuletwa Mkoani Kigoma kama ilivyo adhma ya Serikali ya awamu ya Tano.