Mashirika yanayojihusisha katika utoaji wa huduma mbailmbali za kibinadamu kuwahudumia wakimbizi katika kambi za Wakimbizi Mkoani Kigoma, yameonywa kutokuingilia mchakato wa Zoezi la kuwarejesha kwa hiari wakimbizi walipo katika kambi za Nduta, Mtendeli na Nyarugusu zilizopo Mkoani Kigoma Mkoani Kigoma.
Akiongea na jamii ya wakimbizi katika kambi ya Nduta, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mhe. Brig. Jen. (mst) Emanuel Maganga amesema makundi ama mashirika yanayotoa vitisho kwa wakimbizi wa Burundi waliojiandikisha kurejea nchini mwao kwa hiayari kwa lengo la kuwatishia ili waendelee kuwa wakimbizi kwa manufaa binafsi ya watu au mashirika yatashughulikiwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
Akiwa katika zira ya uhamasishwaji wa wakimbizi kurejea nchini kwao Burundi, Maganga amesema Nchi ya Burundi kwa sasa ina amani na utulivu, matukio yanayotokea ni yale ya kawaida amabayo yanaweza kuwepo katika jamii nan chi yoyote dunia. Amewahakikishia wakimbizi kuwahadi sasa nchi ya Burundi inawakazi zaidi ya Milioni 12 ambao wanaendelea kuishi na kufanya kazi bila bughudha yoyote nchini Burundi.
Maganga ameongeza kuwa yari wakimbizi zaidi ya 38000 wamereja kwa hiayari na kupokelea nchini mwao wanaendele kuishi bila matatizo, hivyo wakimbizi waliopo Mkoani Kigoma hawana budi kuru nchini mwao Burundi kwenda kujenga nchi yao.
Naomba niwaambie ndugu zangu kuwa kambi za wakimbizi siyo makazi ya kudumu, hivyo mnapaswa kurejea nyumbani mkajenge nchi yenu na kuishi kwa heshma alisisitiza Manganga.
Aidha amewaeleza kuwa Serikali ya Tanzania haina mpango wa kutoa Urai kwa wakimbizi kutoka Nchi ya Burundi, vilevile mpango wa kuhamishiwa nchi ya tatu ni finyu kwa sasa na raia wa Burundi hawamo katika mpango huo.
Kwa upande wao Baadhi ya Wakimbizi wametupia lawama kwa Shirika la Kuhudumia wakimbizi pamoja na Mashirika mengine ya nayohusika na kusafirisha wakimbizi wakati wa kurejea kwao kuwa wamekuwa wakijiandikisha kurejea kwa hiari nchini kwao, lakini wanakaa miezi sita hadi minane hawarudishi jambo ambalo limekuwa wakati mwingine likiwakatisha tama.
Nkeshimana Irankunda akiongea mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ameeleza kuwa wakimbizi wengi wameonesha nia ya kurejea nchini Burundi kwa hiari ili kwenda kujenga nchi yao, lakini wanapojiandikisha utaratibu wa kusafirishwa umekuwa na mlolongo mrefu kiasi cha kuwakatisha tama na kubadirisha nia yao ya kurejea.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa