Mashindano michezo ya UMISSETA yameanza kurindima katika viwanja vya Chuo cha Ualimu Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma yakihusisha jumla ya wanamichezo 568 kutoka katika Halmashauri sita Nane za Mkoa wa Kigoma.
Kuanza kwa mashindano hayo kimkoa ni njia ya Kuelekea kupata timu ya Mkoa ambayo itapeperusha bendera ya Moa wa Kigoma katika Mashindano hayo yatakayofanyika Kitaifa Jijjini Mwanza.
Michezo inayoshindaniwa ni Soka (Wavulana na Wasichana), Mpira wa Mikono (Wavulana na Wasichana), Mpira wa Pete, Mpira wa kikapu (wavulana na wasichana), Mpira wa wavu (wavulana) Riadha na Fani za ndani (kwaya, Ngoma, Ngojera na Mashairi)
Lengo la mashindano haya ni kuibua vipaji kupitia kauli mbiu isemayo;
“Michezo Sanaa na Taaluma ni msingi wa maendeleo ya mwanafunzi katika maendeleo ya Taifa letu”.
Akifungua mashindano Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brig. Jen. (Mst.) Emmanuel Maganga amewaasa wanamicheo kuwa na nidhamu kwa watu wote na kuonesha bidii na juhudi katika michezo mbalimbali watakayocheza.
Sambamba na hilo Maganga amesema ili michezo mbalimbali iweze kuimarika hapa Tanzania, ni wakati sasa wa kuibua vipani mbalimbali kupitia UMISSETA kwani vijana wengi wanauwezo ila wanakosa muendelezo wa vipaji vya michezo walivyonavyo.
Mashindano ya UMISSETA kitaifa yatafunguliwa tarehe 4 Juni, 2018 kwenye viwanja vya michezo vya Chuo cha Ualimu Butimba Jijini Mwanza. amapo yatafanyika tarehe 15 Juni, 2018 hadi tarehe 16 Juni,
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa