Vashiria vya ugonjwa wa Malaria nchini Tanzania vimepungua kwa watoto chini ya miaka mitano kutoka14.4 % mwaka 2015 na kufikia 7.3% kwa Mwaka 2017 hii ni kufuatia harakati zinazofanywa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Mashirika ya Marekani (USAID) pamoja na shirika la afya duniani WHO kuhakikisha ugonjwa huo unatokomezwa nchini.
Akizindua takwimu za kitaifa za Matokeo ya Utafiti wa Viashiria vya Malaria kwa Mwaka 2017 zilizotolewa na ofisi ya Takwimu Tanzania leo Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma,Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na cha watoto wenye malaria ni, Kigoma (asilimia 24.4), Geita (asilimia 17.3), Kagera (asilimia 15.4) na Tabora (asilimia 14.8) ambapo Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Njombe, Songwe na Dodoma ina kiwango kidogo cha maambukizi chini ya asilimia moja.
Naye Mkurugenzi mkuu ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Albina Chuwa alithibitisha Matokeo ya sasa ya utafiti huu, yanaonesha kuwa kiwango cha malaria kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano nchini Tanzania kimeshuka kwa zaidi ya nusu kutoka asilimia 14.4 mwaka 2015 hadi asilimia 7.3. hii ni kwa kutumia kipimo cha haraka cha utambuzi wa vimelea (mRDT).
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa