Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye ameyataka makundi mbalimbali kujitokeza kushiriki katika kazi za maendeleo kama Sehemu ya kuonesha uzalendo kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanzania.
Andengenye amesema amesema hayo alipotembela kukagua ujenzi wa kituo cha afya kijiji cha Kagondo katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu.
Amesema katika kushiriki shughuli za maendeleo UVCCM, Mgambo,UWT wana nafasi kubwa ya kujipangia ratiba za kushiriki kufanya kazi. Za ujenzi wa Zahanati ya Kagondo.
Maendeleo tunayoyaona leo ni Sehemu ya wazee wetu ambao walijitoa kwa ari na uzalendo kushiriki katika kuijenga Tanzania ambayo leo tunashuhudia hatua kubwa ya maendeleo katika sekta zote.
Tunachopaswa kama watanzania ni kuendelea bkutunza na kulinda amani yetu ya Tanzania ambayo ni tunu muhimu tuliyoachiwa na Waasisi wa taifa hili.
Tnaposherekea miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania hatuna budi kuendelea kuunga Mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita yenye nia thabiti ya kuyaendeleza mawazo na ndoto za watangulizi wake.
Katika ziara yake Andengenye amekagua miradi ya maendeleo na kushiriki katika shughuli za miradi mbalimbali ya afya, na Elimu.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa