WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KASSIM MAJALIWA AKZINDUA RASMI ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA MKOANI KIGOMA.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezindua zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura huku akiwataka watanzania wote kujitokeza kujiiandikisha na kuboresha taarifa zao katika daftari hilo.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo wa daftati la kudumu la wapiga kura uliofanyika uwanja wa Kawawa manispaa ya Kigoma Ujiji Waziri Mkuu Majaliwa alisema kuwa zoezi la uboreshaji wa daftari kudumu la Wapiga kura na zoezi zima la Wapiga kura linawuhusu watanzania kulingana na kutambuliwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alisema kuwa taarifa za tume huru ya Taifa ya uchaguzi (INEC) inaonyesha kuwepo kwa wapiga kura wapya milioni 5.5 ambao wanapaswa kuandikishwa kulingana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 hivyo tume imejiandaa kuhakikisha watu wote hao wanaandikishwa katika zoezi la kuandikisha.
Sambamba na hili Waziri Mkuu Majaliwa amewataka Watanzania wote kusimamia kwa karibu utekelezaji wa zoezi hilo wakiwemo mawakala kuhakikisha wanaondikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ni Watanzania ili wapate nafasi ya kuchagua viongozi wao na kuwafichua watu ambao siyo watanzania wanaotaka kujipenyeza kuandikishwa.
Pamoja na hilo alisema kuwa uandikishwaji mwaka huu umeboreshwa kwa kiasi kikubwa ambapo zoezi hilo unaanzia kwenye simu ya mkononi ya kila Mtanzania hivyo watekeleze hilo ili kupunguza msongamano, kupunguza muda wa kukaa vituoni na kulifanya zoezi kuwa rahisi.
Aidha katika uzinduzi huo Waziri Mkuu Mkuu amevitaka vyama vya siasa ambao ndiyo wadau wakubwa wa uchaguzi huo kutoa elimu kwa wanachama wao kuhusu zoezi hilo lakini pia kuweka mawakala ambao watasimamia zoezi hilo kwenye vituo akitaka mawakala hao kutolewa kwenye maeneo husika ya vituo na kuwa na uzalendo na nchi yao.
Waziri Mkuu Majaliwa pia ameyaasa mashirika yasiyo ya serikali yaliyoteuliwa kutoa elimu kwenye zoezi la uandikishaji na uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kuzingatia majukumu yao kulingana na maombi yao na zoezi lenyewe badaya la kufanya mambo ambaayo hayasiaani na taratibu za daftari wala uchaguzi.
Katika uzinduzi wa zoezi hilo Waziri Mkuu Majaliwa alitoa agizo kwa idara ya uhamiaji mkoa Kigoma na nchi nzima kwa jumla kutembelea vituo na kufanya uhakiki wa watu wanaoandikishwa kuwa ni Watanzania na kufanya kazi taarifa watakazopata kuhusu watu wanaotaka kujiandikisha ambao siyo Watanzania
Awali akitoa taarifa kwa Waziri Mkuu, Mwenyekiti wa Tume huru ya Taifa ya uchaguzi nchini (INEC), Jacob Mwambegele alisema kuwa Katika uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mwaka huu 2024 kutakuwa na jumla ya vituo 40,126, ambapo kati ya vituo hivyo, 39,709 ni vya Tanzania Bara na vituo 417 ni vya Zanzibar.
Jaji Mwambegele alisema kuwa hilo ni ongezeko la vituo 2,312 ikilinganishwa na vituo 37,814 vilivyotumika kuandikisha wapiga kura mwaka 2019/2020 huku kukiwa na ongezeko la wapiga kura wapya milioni 5.5,wapiga kura milioni 4.3 wataboresha taarifa zao na wapiga kura 594,494 wataondolewa kwenye Daftari kwa kukosa sifa za kuendelea kuwepo kwenye Daftari hivyo baada ya uboreshaji inatarajiwa kuwa Daftari litakuwa na jumla ya wapiga milioni 34.7.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa