Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Leo Februari 27, 2023 amehitimisha ziara yake ya kikazi mkoani Kigoma kwa kutembelea na kukagua kiwanda cha kukausha Mbegu za Chikichi (SIDO) pamoja na Kiwanda cha kusindika Mafuta ya Mawese Trolle Messle katika eneo la SIDO Manispaa ya Kigoma-Ujiji.
Mara baada ya ukaguzi huo, Waziri Mkuu alipata fursa ya kuzungumza na viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama cha Mapinduzi pamoja na wananchi ambapo alipokea Taarifa za Mafanikio na Changamoto mbalimbali zinazohusu utekelezaji wa mpango mkakati wa Kilimo cha zao la chikichi mkoani Kigoma, kisha kutoa ushauri na maelekezo kwa Idara na Taasisi zinazohusika ili kupata utatuzi wa changamaoto hizo.
Aidha Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kupiga marufuku wafanyabiashara wa Mafuta ya mawese kutumia madumu yaliyozidi vipimo halisi (mabidoo) katika masoko ya bidhaa hiyo mkoani Kigoma.
Matumizi ya mabidoo ni unynyaji mkubwa unaofanywa na wafanyabiashara kwa lengo wa kujipatia faida kubwa huku wakiwaacha wakulima wakipata hasara kutokana na kutumia vipimo hivyo visivyo sahihi.
Ziara hiyo ya Waziri Mkuu ilianza kwa kukutana na wadau wa Kilimo cha chikichi kwa lengo la kufanya Tathimini ya Mafanikio yaliyofikiwa katika kuanzisha, kuendeleza na kuboresha kilimo cha zao la chikichi mkoani hapa.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa