Jaji mfawidhi Mahakama kuu Tabora(Salvatory Bongole) amewasili Mkoani Kigoma kumkabidhi rasmi Jaji Mfawidhi Mahakama kuu Kigoma(Irvin Claud Mugeta) ili ianze kuwahudumia wananchi wa Kigoma. Makabidhiano ya Mahakama kuu Mkoani Kigoma ni historia mpya na kubwa ya kimageuzi katika Suala zima la kuhakikisha wananchi wanaondokana na adha ya kusafiri kwenda Mkoani Tabora kufuata hudumu za Kimahakama, vilevile itarahisisha upatikanaji wa haki kwa wakati na kupunguza gharama kama ilivyokuwa hapo awali. Hongera Kwa wanakigoma, na pongezi kwa Serikali ya awamu ya tano kwa kuijali Kigoma.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa