MKUU WA KITENGO CHA TEHAMA KATIKA OFISI YA MKUU WA MKOA WA KIGOMA ASHURA SADICK, AKIWASILISHA MADA KWA WAJUMBE (HAWAPO PICHANI) KUHUSU NAMNA YA KUTUMIA MFUMO MPYA WA UNUNUZI SERIKALINI (NeST). MAFUNZO HAYO YANAFANYIKA KATIKA UKUMBI WA OFISI YA MKUU WA MKOA WA KIGOMA.
BAADHI YA WAKUU WA IDARA NA VITENGO VYA HALMASHAURI NANE ZA MKOA WA KIGOMA WAKIFUATILIA JAMBO WAKATI WA UFUNGUZI WA MAFUNZO YA MATUMIIZI YA MFUMO MPYA WA UNUNUZI SERIKALINI (NeST) YANAYOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA OFISI YA MKUU WA MKOA WA KIGOMA.
Wataalam kutoka Idara na Vitengo katika Halmashauri Nane za Mkoa wa Kigoma wametakiwa kuzingatia mafunzo ya Mfumo wa Manunuzi Serikalini (NeST) ili kuongeza Tija katika eneo hilo muhimu la utoaji Huduma kwa Umma.
Wito huo umetolewa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Patrick Kigere alipofungua mafunzo ya Siku Tano kwa wataalam hao yaliyolenga kuwajengea uwezo katika matumizi ya mfumo huo mpya wa Manunuzi serikalini yanayofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kigoma.
Amesema Serikali kupitia Mamlaka ya kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) imeamua kuimarisha mifumo pamoja na taratibu za manunuzi serikalini kwa lengo la kudhibiti changamoto zinazozikabili Taasisi nunuzi pamoja na wazabuni.
‘’Katika Mafunzo haya, mtajengewa uwezo ili kupata weledi katika kutumia mfumo na mkazingatie yale mnayojifunza kwenye utendaji wenu na kutokwenda kinyume na matakwa ya Serikali’’ amesisitiza Kigere.
Aidha Kigere amesema kukamilika kwa mafunzo hayo kukawe chachu na kutia msukumo kwa taasisi za Ummamkoani Kigoma kuanza kutumia mfumo ifikapo Oktoba 1, 2023.
KAIMU KATIBU TAWALA MKOA WA KIGOMA PATRICK KIGERE AKIZUNGUMZA NA WAKUU WA IDARA NA VITENGO KUTOKA HALMASHAURI ZA WILAYA ZA MKOA WA KIGOMA (HAWAPO PICHANI) KABLA YA KUFUNGUA MAFUNZO YA MATUMIZI YA MFUMO WA NeST, LEO AGOSTI 28, 2023.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa