KATIBU TAWALA MKOA WA KIGOMA HASSAN RUGWA AKIZUNGUMZA KABLA YA KUZINDUA RASMI KAMBI YA AWAMU YA TATU YA MADAKTARI BINGWA WA MAMA SAMIA MKOANI KIGOMA
BAADHI YA MADKARI BINGWA WA DKT. SAMIA SULUHU WAKIMSIKILIZA KATIBU TAWALA MKOA WA KIGOMA (HAYUPO PICHANI)ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA KABLA YA KUFUNGUA RASMI KAMBI YA SIKU SITA YA MATIBABU YA KIBINGWA MKOANI KIGOMA
Zaidi ya Madaktari bingwa hamsini wa fani nane tofauti kutoka hospitali mbalimbali hapa nchini wameanza rasmi Kambi ya matibabu ya kibingwa mkoani Kigoma ili kusogeza huduma hizo karibu na Wananchi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kambi hiyo maarufu kambi ya Madaktari wa Mama Samia, Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa amesema pamoja na utoaji huduma za kibingwa uwepo wao ni fursa kwa madaktari bingwa wa mkoa wa Kigoma kuongeza ujuzi.
Amewataka wakazi kuendelea kutumia fursa ya uwepo wa kambi hizo kwa ajili ya kupata huduma muhimu za kitabibu katika Hospitali zilizopo katika Halmashauri zao.
Upande wake Mganga Mkuu wa mkoa wa Kigoma Damas Kayera amesema maandalizi yameshafanyika na wataalam hao watazifikia halmashauri zote nane za mkoa.
Mratibu wa Kambi Hiyo kutoka Wizara ya afya Dk. Grace Malick amesema pamoja na huduma zitakazotolewa na madaktari hao, madaktari wenyeji watumie fursa hiyo kujijengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi wao.
Kambi hiyo ya Siku Sita iliyoanza leo Julai 16 hadi 21, 2025 ni ya awamu ya tatu huku kambi zilizopita zikiwa zimafanikiwa kutoa huduma kwa wananchi zaidi ya elfu tano kupitia utoaji matibabu ya kibingwa.
Aidha matibabu yanayotolewa yanahusu magonjwa ya wanawake na ukunga, watoto na watoto wachanga, magonjwa ya ndani, upasuaji na matibabu ya mfumo wa mkojo, huduma za kibingwa kwa ajili ya usingizi na ganzi, matibabu ya kinywa na meno pamoja na mfumo wa pua na masikio.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa