TAHARIRI.
Maboresho makubwa yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika katika Jengo la Ofisi ya Mkoa wa Kigoma pamoja na Ujenzi wa Ofisi na Makazi ya viongozi katika Halmashauri zote za Mkoa wa Kigoma ni Jambo linalopaswa kupongezwa kwani Mazingira Bora ya watoa huduma na utoaji huduma hudumisha upatikanaji wa huduma yenye ubora, utimilifu na yenye kuridhisha.
Ukarabati Mkubwa uliofanyika katika Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa umegusa Maeneo ya ndani na nje ya Jengo na kuyafanya kuvutia kwa watoaji pamoja na wapokea huduma, hali inayosababisha kutochoshwa na Mazingira hayo.
Mpangilio mzuri wa Mandhari ya nje ya Jengo hilo unaruhusu wahitaji wa huduma pamoja na wageni mbalimbali wanaofika katika eneo hilo kutokumbana na adha au usumbufu katika kuzifikia Ofisi, kukutana na watumishi pamoja na kuegesha vyombo vyao vya usafiri katika eneo lenye hadhi na usalama zaidi.
Nitumie fursa hii kutoa pongezi kwa maono makubwa ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Albert Msovela kwa kuguswa na kuyatazama kwa jicho la pili mahitaji ya watoa na wahitaji wa Huduma kupitia Ofisi hii muhimu ya Serikali katika Mkoa wa Kigoma.
Shime kwa watumishi wote wa Umma katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma wenye jukumu la kuwahudumia wananchi, kuongeza ufanisi katika kuhakikisha Mazingira haya yanaendana na kasi ya utoaji huduma yenye ubora na kupatikana kwa wakati. Hilo likifanyika litashabihiana na Dhamira ya Uongozi wa Ofisi katika kufanya maboresho hayo makubwa.
‘’Kazi iendeleee’’
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.
Baadhi ya watumishi wa Sehemu na Vitengo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma wakitekeleza majukumu yao ya kila siku kwa lengo la kuwahudumia wananchi wa Mkoa wa Kigoma
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa