#1.Kuimarisha ulinzi na usalama kwa wananchi-maeneo mengi wananchi wanalalamikia tishio la usalama kwa sababu ya uwepo wa wakimbizi wegi katika kambi za Nduta na Mtendeli
#2. Wananchi na Maafisa/watumisi wasio na Mafunzo ya Mgambo wajiunge na Mafunzo ya Mgambo
#3. Suala la uadikishwaji wa Vitambuliso vya Utaifa lifanywe kwa uangalifu ili kuepuka kutoa vitambuliso kwa watu wasio watazania, hii ni pamoja na kutoa elimu ya uraia kwa wananchi kabla ya zoezi lenyewe.
#4. Wananchi wahimizwe kujiuga na bima ya Afya CHF kwa kauli ya Kuku mmoja matibabu Mwaka mzima kwa familia
#5. Vijana na Kinamama wapatiwe elimu juu ya umuhimu wa kujiunga kwenye vikundi ili kupata mikopo kupitia fedha za Halmashauri 10% ya makusanyo ya ndani
#6. Watendaji wasikae Ofisini, waende vijijini kuwahudumia wananchi
#7. Halmashauri zitengeneze mabwawa ya samaki kwa kila shule kama sehemu ya Mafunzo na lishe kwa wanafunzi
#8. Shule zipewe maeneo ya kilimo kama shamba darasa na Chakula cha shule
#9. Elimu bila malipo: pale penye uhitaji wa michango utaratibu ufuatwe kupitia vikao vya wazazi na bodi za shule
#10. Miundombiu ya shule ilindwe na kutunzwa, bajeti za walinzi ziwekwe
#11. Jeshi la polisi imarisheni ulizi komeshei kabisa matukio ya utekaji Mkoani Kigoma
#12. Kamati za Maji za vijiji ziimariswe na kusimamiwa ili kutoa huduma bora za maji vijijini
#13. Tovuti za almasauri zifanyekazi kutoa taarifa kwa wananchi/umma
#14. Hali ya Mapambano dhidi ya rushwa inaridha kwa sasa Mkoani Kigoma lakini juhudi zaidi ziongezwe ili kutokomeza adui huyu
#15. Walimu waliohamishwa lakini bado hawajaenda katika vituo vyao waripoti ndani ya siku saba wasipofanya hivyo sheria ifanye kazi
#16. Viongozi waepuke migogoro ya chuki na maslahi binafsi, badala yake wachape kazi kwa maendeleo ya wananchi
#17. Watendaji na Watumishi tendeni haki kwa wateja wenu ambao ni wananchi
#18. Tunapohimiza michango ya madawati na maendeleo mengine watumishi na Watendaji wawe mstari wa kwanza kuchangia
#19. Taasisi za Umma hususani shule na Hospitali ziwekewe “thunder arrester” vizuia radi kupunguza vifo vinavyosababshwa na radi
#20. Taasisi zote zilipe kodi kwa watoa Huduma kwa kuzingatia sheria
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa