Maafisa Ustawi wa Jamii waaswa kufanya kazi zao kwa weledi kuwahudumia wahitaji
Viongozi wa Serikali na Watendaji wakuu kwenye Mkoa na mamlaka za Serikali za Mitaa wametakiwa kushirikiana na wadau mbalimbali suala la utoaji huduma kwa jamii ikiwemo masuala ya makundi maalumu hususan wazee na walemavu.
Ameyasema haya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brig. Jen. (mst.) Emmanuel Maganga wakati wa kuzindua mradi wa kuboresha ulinzi wa usawa, ustawi na usalama wa watu wenye mahitaji maalumu (wazee na walemavu) unaotekelezwa na Shirika lisilo la kiserikali la HelpAge.
Wakurugenzi wa Halmashauri kupitia kwa wataalamu wenu wa Ustawi wa Jamii, nendeni mkasimamie utekelezaji wa moja kwa moja wa mradi huu kwa kushirikiana na HelpAge katika Halmashauri zenu. Uwepo Mabaraza ya Ushauri ya wazee ngazi za Vijiji/Mitaa, Kata, Halmashauri na sasa Mkoa basi ikawe ni chachu katika kutekelezeka kwa mradi huu kwani mabaraza haya yatasaidia katika kufanikisha azma hii nzuri ya mdau amesema Mkuu wa Mkoa.
Maafisa ustawi wa jamii wakafanye kazi kubwa kwenye kuwajengea uwezo wazee, kuyajengea uwezo mabaraza, kuwawezesha wazee na mabaraza yao kutimiza majukumu yao kwenye jamii ili hatimae wazee na walemavu wakapate wepesi katika kupata huduma zao.
Aidha amewapongeza Shirika la HelpAge kwa kuwekeza katika kuhudumia kundi maalumu la wazee na walemavu kwa kumekuwa na changamoto kubwa ya wadau wengi kutowekeza au kutoa huduma kwa makundi haya mawili muhimu kwenye Mkoa wetu na hata nchi nzima kwa ujumla, hivyo tunapompata mdau ambaye anaonyesha nia dhahiri kama HelpAge, sisi kama serikali ni kuhakikisha tunashirikiana nae ili kufanya wepesi katika utekelezaji wa mradi na hatimae matokeo yake yaweze kuonekana mapema amesisitiza Mkuu wa Mkoa.
Naye Mratibu wa Mradi wa HelpAge Bw. Leonard amefafanua kuwa wamedhamiria kufanya kazi katika maeneo makuu matatu kama kwenye uimarishaji wa huduma za afya kwa walengwa, kutetea haki za wazee na walemavu na pia kusaidia kutilia mkazo eneo la hifadhi ya jamii.
Aidha, maeneo haya matatu ni muhimu kwa makundi hayo kwenye jamii kwani ndiyo maeneo ambayo kama yatafanyiwa kazi kwa juhudi na mdau mbalimbali, kwa sehemu kubwa itasaidia kutatua changamoto zinazowakabili wazee na walemavu kwenye jamii yetu ya Mkoa wa Kigoma.
Mpaka sasa shirika la HelpAge lomekwisha tekeleza kiraqdi mbalimbali Mkoani Kigoma ikiwemo uwezeshaji mkubwa kwenye halmashauri za Kakonko na Kibondo, kutoa baadhi ya huduma kwenye kambi ya wazee Kibirizi na kuundwa kwa mabaraza ya wazee kwenye halmashauri na Mkoa.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa