Wakazi katika Kata ya Mwamgongo na Kagunga zilizopo Halamashauri ya Wilaya ya Kigoma mkoani hapa wameishukuru serikali kwa kuimarisha huduma za utoaji wa huduma ya kingatiba kupitia utaratibu wa kutoa chanjo kwa ajili ya kudhibiti magonjwa mbalimbali hali inayochangia ulinzi wa Afya za watoto wao na kudumisha Afya bora kwa watoto ili kuimarisha nguvu kazi ya Taifa kwa siku zijazo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti waliposhiriki katika zoezi la kuhamamasisha chanjo lililofanyika wilayani Kigoma likihusisha Kamati za Afya Mkoa na wilaya ya Kigoma kwa ufadhili wa Shirika la Uhamiaji (IOM) wameipongeza serikali kwa kuendelea kuhakikisha huduma za chanjo zimekuwa zikiwafikia kwa wakati na kupatikana bila uwepo wa changamoto zozote pamoja na maeneo yao kuwa na changamoto ya kufikika kw a urahisi.
Fatuma Ibrahim Mkazi wa Kijiji cha Mwamgongo amesema huduma ya chanjo imekuwa ikipatikana kwa wepesi katika zahanati iliyopo kijijini humo jambo linalowahakikishia ulinzi na usalama wa Afya za watoto wao.
Hamimu Sudi Mkazi wa Kijiji cha Mwamgongo mesema kupitia utaratibu wa hamasa unaoendeshwa na wataalam wa Afya kutoka serikalini kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo unachangia kwa kiasi kikubwa wananchi kushiriki katika kupata huduma hiyo jambo linalopunguza athari za magonjwa ambapo matokeo yake ni vifo na ulemavu kwa watoto.
Mratibu wa Huduma za chanjo Mkoa wa Kigoma Yohanes Peter amesema mkoa umeadhimisha wiki ya chanjo kitaifa kwa kuendesha huduma za mkoba kwa ajili ya kuwafikia walengwa huduma za chanjo ambao ni mabinti wenye umri wa miaka chini ya Tisa, watoto wenye umri chini ya miaka mitano na wanawake walio katika umri wa kujifungua ikiwa ni mika 15 hadi 45, ambapo zoezi hilo linafanyika kwa kutembelea maeneo yote ya mkoa yenye changamoto ya kufikika kwa urahisi ili kuongeza uelewa na hamasa ya umuhimu wa chanjo kwa jamii.
Amesema kwa Halmashauri ya Kigoma wamefanikiwa kuzifikia kata za Kagunga, Zashe na Kata ya Mwamgongo ambapo zoezi kubwa lililofanyika ni kuhamasisha wakazi kujitokeza, kushiriki kupewa elimu pamoja na kuendesha zoezi la utoaji chanjo kwa kushirikiana na wataalam wa Afya waliopo katika maeneo hayo.
Amesema sambamba na hayo kazi nyingine zilizofanyika ni upimaji wa uzito, shinikizo la damu pamoja na ushauri wa kiafya.
Zoezi hilo ni mwendelezo wa maadhimisho ya Wiki ya chanjo duniani kuanzia Aprili 24-30,2025 ambapo maadhimisho ya kitaifa kwa mwaka huu wa 2025 yatafanyika mkoani Dodoma,
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa