MKUU WA MKOA AAGIZA WALIOISABABISHIA HATI CHAFU MANISPAA YA KIGOMA UJIJI WACHUKULIWE HATUA
Posted on: August 3rd, 2017
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali (Mst.) Emmanuel Maganga ameuagiza uongozi wa Manispaa ya kigoma/ ujiji kuwachukulia hatua za kisheria watumishi waliohusika katika ubadhirifu na wizi wa fedha na kupelekea Manispaa hiyo kuwa na hati chafu kwa mfululizo wa miaka miwili 2014/2015 na 2015/2016.
Mhe. Maganga ameagiza kuwu tarifa ya hatua za kinidhamu na kiutawala iwasilishwe katika ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa ndani ya Miezi Miwili kuanzia leo yaani siku 60.
Akizungumza katika Kikao cha Baraza la Madiwani katika Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkuu wa Mkoa Maganga amesema malalamiko na migogoro mingi inasababishwa na utendaji mbovu wa baadhi ya watendaji na watumishi na wengine wakijificha katika mgongo wa madiwani katika kutenda kinyume na taratibu za kiutumishi.
Mwenendo wetu kiutendaji haubadiliki tunapaswa kubadilika ili kuleta matokeo chanya kwa wananchi. Waheshimiwa madiwani na watendaji tufanye kazi kwa malengo na zejye kupimika. Aliongeza Maganga.
Aidha Maganga ametoa maelekezo mbalimbali ikiwemo kuacha kutengeneza shughuli nje ya bajeti iliyoidhinish, madiwani kuacha kujihusisha na masuaa ya utendajimathalani zabuni na biashara na Halmashauri pamoja na kujiepusha kuingila michakato ya zabuni inayoendeshwa na Bodi ya Zabuni ya Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Zipo taarifa kuwa baadhi ya madiwani wanalinda watumishi wasio waadilifu ili wasichukuliwe hatua za kisheria na kinidhamu pindi wanapogundulika na makosa hili haikubaliki kabisa alisisitiza Brigedia Jenerali Maganga.
Amekemea vikali suala la watendaji na watumishi kujihusisha na malipo yasiyofuata taratibu za sheria ya fedha.Aidha amewataka kusingatia hoja na maelekezo ya Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ili kuondokana na kupata hati chafu. Amesema haiwezekani hoja zote saba zikepelekea kupata hati chafu kwa miaka miwili mfululizo hali hii haivumiliki, wote waliohisika wawe wamehama katika Manispaa hii au wamestaafu watafutwe na waletwe kujibu hoja hizi.
Mhe. Mkuu wa Mkoa amevielekeza vyombo husika kuharakisha upelelezi ili hatua stahiki zichukuliwe kwa watakaobainika kutenda makosa hayo.
Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Kigoma Ujiji ambacho kilikuwa na agenda mojo tu ya Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikalikilihudhuriwa pia naZito Zuberi Kabwe ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma mjini amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kwa kutoa maagizo na maelekezo mbalimbali na kuomba yasimamiwe na yatekelezwe ili kuondoa aibu ya Manispaa ya kupata hati chafu.
Mhe. Zitto amesema yeye hatamwonea aibu Mtumishi au diwani yeyote anayekwamisha maendelo ya Manispaa. Amewataka madiwani bila kujali itikadi ya vyama kuunga mkono jitihada za serika za maendeleo kwa wananchi, pia kutooneana aibu kwa wanaokwenda kinyume na taratibu ikiwemo wizi na ubadhirifu wa fedha za umma.