Jumla ya Dola za Kimarekani 55 milioni zinatarajiwa kutumiwa katika miradi mbalimbali mtambuka katika Mpago wa pamoja wa Umoja wa Mataifa kwa Mkoa wa Kigoma.
Hadi sasa Shiling 15 milioni zimekwisha kutolewa na Serikali za Norway, na Korea ili kuanza utekelezaji wa Miradi mbalombali ya Maendeleo katika Mkoa wa Kigoma. Miradi mingi imelengwa kutekelezwa hasa katika maeneo ya Elimu, Afya, Kilimo, Uwezeshaji wa Kibiashara kwa kinama na Vjana wajasliamali.
Akifungua warsha ya pamoja ya ya Mpango wa Pamoja wa Umoja wa Mataifa kwa Mkoa wa Kigoma.Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brig. Jen. (Mst.) Emmanuel Maganga amesema miradi mbalimbali imelenga kuinua wananchi kiuchumi, hivyo amesisitiza ninfursa nzuri kwa wananchi wa Kigoma kutumia miradi hii kwamaendeleo. Miradi mingine itakayotekelezwa ni pamoja na kujenga masoko ya mipakani.
Mkuu wa Mkoa mesisitiza kuwa miradi yote isimamiwe kwa umakini ili kuleta tija kwa wananchi hasa kubadili maisha yao kiuchumi
Naye Mratibu wa Mpango wa Pamoja wa Umoja wa Mataifa Bw. Evance Siangicha ameeleza kuwa mradi umelenga hususan Wilaya za Kasulu, Kibondo na Kkonko ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikipokea wakmbizi hivyo kufanya.
Aidha, ameeleza kuwa mbali na miradi ya kimaendeleo, mradi pia utajihusisha katika masuala ya kijamii mazingira, haki za binadamu.
Mradi wa Pamoja wa Umoja wa Mataifa kwa Mkoa wa Kigoma unatekelezwa chini ya ufadhili wa Umoja wa Mataifa kupitia Mashirika 16 yaliyop nchini Tanzania.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa