Kiwango cha maambukizi ya ugonjwaa wa Malaria mkaoani Kigoma kimeendelea kushuka kufuatia utekelezaji wa zoezi la unyunyiziaji wa Kiuatilifu ukoko majumbani lililofanywa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Abt Associates katika Halmashauri za Wilaya Kasulu na Kibondo.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye amesema Takwimu zinaonesha kuanzia Mwaka 2018 hadi 2021 maambukizi yameendelea kushuka kutoka Asilimia 33.1 hadi 12.5 kwa wilaya ya Kasulu na Asilimia 24.1 hadi 12.5 kwa wilaya ya Kibondo.
Kupitia kikao cha uhamasishaji zoezi la upuliziaji kiuatilifu ukoko majumbani kilichofanyika mkoani hapa, Mkuu wa Mkoa amewaelekeza wakuu wa wilaya na wakurugenzi kutenga bajeti ya manunuzi ya viuadudu vya kibaiolojia na kuhakikikisha huduma bora na elimu dhidi ya maambukizi ya Malaria zinaendelea kutolewa kwa Jamii.
Serikali iliazimia kufanyika kwa zoezi hilo katika wilaya za Kasulu na Kibondo mkoani Kigoma, kufuatia takwimu kuonesha maambukizi makubwa ya ugonjwa wa Malarial ambapo kwa kila watu 1000 waliobainika na maambukizi kwa wilaya ya kibondo ni 203.9 na Kasulu ni 155.3.
Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Shirika lisilo la kiserikali la Abt Associates kupitia Mradi wa VectorLink Tanzania wanatarajia kuendesha zoezi la upuliziaji kiuatilifu ukoko majumbani katika wilaya za Kibondo na Kasulu Mwezi Oktoba 2022.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa