Mkoa wa Kigoma umejipanga kufanya vizuri kimichezo katika Mshindano yajayo ya Umoja wa Michezo kwa Shule za Msingi (UMITASHUMTA) na Sekondari (UMISETA) na kuendelea kuibua vipaji mbalimbali vya wanamichezo kwa manufaa ya Taifa na kuongeza Fursa ya Ajira kwa vijana.
Afisa Maendeleo ya Vijana Mkoa, Edward Manase amesema kwa sasa wanajipanga katika kuongeza nguvu kwenye kutumia wataalam na wabobezi katika Fani mbalimbali za Michezo ili kusaka vipaji kuanzia ngazi za vijiji, kata, wilaya mpaka Mkoa na kuunda timu zenye Ubora zitakazoleta ushindani zaidi katika ngazi ya mashindano hayo kitaifa.
Aidha amekiri kuwepo kwa malalamiko kuhusu taratibu zinazotumika katika kuchagua na kupata wanamichezo wanaounda timu ngazi za kata, wilaya hadi Mkoa kwa ajili ya kushiriki Mashindano ya Umoja wa Michezo kwa Shule za Msingi na Sekondari na kusema kuwa, taratibu za uchaguzi wa wachezaji hao hufanywa kwa kuzingatia miongozo iliyowekwa.
Amesema baadhi ya Wilaya hushindwa kuandaa timu kwa baadhi ya Michezo kutokana na kukosa wataalam au wajuzi wa michezo hiyo jambo linalosababbisha kukosa uwakilishi kimkoa.
‘’Baadhi ya maeneo Muamko wa kimichezo upo juu mfano maeneo ya mjini ambapo vijana hushiriki michezo mbalimbali tofauti na maeneo ya vijijini, hali inayosababisha linapofanyika zoezi la kuunda timu za Mkoa, wale wa mjini huonekana kufanya vizuri zaidi na kujitokeza katika michezo tofauti tofauti ikilinganishwa na wanaotoka maeneo ya vijijini’’ amesema Manase.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa