Halmashauri zote Mkoani Kigoma zimetakiwa kuainisha malighafi zote zinazopatikana katika maeneo yake, pamoja na kutambua fursa zilizopo na namna ya kuwasaidia wananchi kuanzisha viwanda ili kutekeleza sera ya viwanda 100 Mkoani Kigoma.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Emannuel Maganga akizungumza katika Mkutano wa pili mwaka 2017 wa baraza la uwezeshaji biashara la Mkoa, ili kutekeleza sera ya viwanda 100 Mkoani Kigoma viongozi na watendaji waache kufanya mambo kwa mazoea watumie taaluma na weledi kubuni mambo yatakayowasaidi wananchi kuanzisha viwanda na pia kuzalisha bidhaa zenye ubora hivyo kila Halmashauri hainabudi kuwa na mipango mkakati ambayo sit u itabaki kwenye maandishi bali kwenye utekelezaji na utendaji hatimaye wananchi waweze kufaidika.
Maganga alisema Mkoa wa Kigoma unamalighafi nyingi ambazo ni fursa kwa wananchi kuanzisha viwanda vya kuchakata malighafi hizo na kuziuza ndani ya nchi na nchi jirani za Kongo na Burundi.aliongeza kuwa changamoto ya umeme isiwe kigezo cha kushindwa kwani viwanda vidogovidogo vinavyotumia umeme wa kawaida vinawezekana kuanzishwa kwa umeme uliopo.
Katika kufanikisha azma ya kufikia Uchumi wa Viwanda Halmashauri zimeshauriwa kutenga fedha za kutosha kila mwaka katika bajeti zake ili kuhakikisha kuwa zinajenga na kuboresha mazingira bora yatakayo wavutia zaidi wawekezaji hasa sekta binafsi kuwekeza katika sekta ya viwanda
Aidha amezitaka taasisi za kifedha kuangalia namna zinavyoweza kuwawezesha vijana na wajasiriamali katika kufanikisha suala la uwekezaji wa viwanda kwani kwa kufanya hivyo watakuza uchumi wa Mkoa wa Kigoma na nchi kwa ujulma.
Hivi karibuni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Miko na Serikali za Mitaa Mhe. Suleiman Jaffo (Mb) alizindua mpango wa uanzishwaji wa viwanda Mjini Dodoma chini ya kaulimbiu ya Mkoa wangu Kiwanda changu, yenye lengo la kuhakikisha kila mkoa utumie fursa zilizopo kutekeleza azma ya serikali ya awamu ya tano ya nchi ya viwanda.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa