Jamii mkoani Kigoma imeaswa kuendelea kutunza amani na mshikamano uliopo ili kudumisha utulivu hali itakayochochea Maendeleo ya Wananchi.
Wito huo umetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa alipomwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania bara ambapo kimkoa maadhimisho hayo yamefanyika katika Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Amesema kila mtu anao wajibu wa kudumisha umoja na amani ikiwa ni misingi iliyoasisiwa na baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa lengo la kudumisha Maendeleo ya nchi.
Katika hatua nyingine Rugwa amehimiza jamii kuendelea kutunza mazingira ikiwa ni pamoja na kujenga utamaduni wa kupanda miti.
"Katika kutekeleza sera ya utunzaji wa Mazingira, tumejiwekea utaratibu wa kupanda miti Mil. 1.5 kwa kila halmashauri ikiwa ni sawa na miti Mil. 12 kimkoa kwa kila mwaka" amesema Rugwa.
Aidha katika kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania bara, Katibu Tawala Mkoa ameongoza kufanya zoezi la usafi sambamba na kuongoza wananchi kupanda miti katika eneo la Hospitali hiyo ikiwa ni katika kuhamasisha suala la utunzaji wa mazingira.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa