Mkoa wa Kigoma unaendelea kufanya vizuri kitaifa katika uzalishaji wa zao la Muhogo ambapo makadirio kwa Mwaka hufikia hadi Tani Mil. 1.2 za muhogo mkavu na mbichi huku matarajio ikiwa ni kufikia zaidi ya Tani Mil.3 ifikapo mwaka 2030.
Mshauri wa Kilimo Mkoa wa Kigoma Joseph Lubuye, alisema Mafanikio hayo yamechagizwa na matumizi ya mbegu za kisasa aina ya Mkombozi, Kipusa na Tanzania 130 ambazo huchukua muda wa miezi tisa kukomaa tofauti na mbegu za kienyeji ambazo huchukua miaka miwili hadi mitatu huku zikitoa mazao hafifu.
Alitoa ufafanuzi kuwa, uzalishaji wa zao hilo unazidi kuimarika kutokana na matumizi ya mbegu hizo za kisasa ambazo ni kinzani dhidi ya ugonjwa wa batobato na michirizi kahawia inayoathiri uzalishaji wa zao la muhogo.
Lubuye amewataka wanunuzi wa zao hilo kuzingatia sheria zilizowekwa na Serikali ili kuwanufaisha wakulima pamoja na nchi kupata mapato kutokana na Biashara hiyo badala ya kuendelea kuwakatumia madalali ambao huwakandamiza wananchi kwa kujipangia bei ya kununua zao hilo sokoni.
‘‘Wateja wakubwa wa Muhogo unaozalishwa mkoani hapa hutoka katika Nchi za Burundi, Congo, Uganda na Rwanda ambao hununua zaidi ya Asilimia 80 huku Asilimia iliyobakia ukitumika nchini kwa ajili ya chakula’’ alisema Lubuye.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa