MKUU WA MKOA WA KIGOMA KAMISHNA MSTAAFU WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI THOBIAS ANDENGENYE AKIONGOZA KIKAO CHA WATAALAM KUTOKA OFISI YA MKUU WA MKOA, TANESCO, NEMC NA KUWASA PAMOJA NA WATAALAM KUTOKA KAMPUNI YA TAZACO INV. LTD WALIPOMTEMBELEA OFISINI KWAKE KWA LENGO LA KUTAMBULISHA ZOEZI LA UPEMBUZI YAKINIFU WANALOLIFANYA KWA LENGO LA KUANDAA MAPENDEKEZO YA AWALI KWA AJILI YA MPANGO WA UPANUZI WA BANDARI YA KIGOMA APRILI 29,2024.
Wataalam kutoka Kampuni ya TAZACO Investment Limited Tz wamewasili mkoani Kigoma na kukutana na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye kwa lengo la kumsalimia kisha kutambulisha zoezi la upembuzi yakinifu wanalolifanya mkoani hapa ili kuandaa mapendekezo ya Awali ya Mpango kazi wa upanuzi wa Bandari ya Kigoma.
Awali akitoa salamu za ukaribisho, Mkuu wa mkoa amesema mkoa upo zaidi ya tayari kwa ajili ya kupokea wawekezaji ili kutimiza dhamira ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuufanya kuwa kitovu cha uwekezaji na Uchumi kwa ukanda wa Magharibi.
Amesema uboreshaji wa bandari hiyo utarahisisha mchakato wa upokeaji, uhifadhi na usafirishaji wa mizigo katika bandari kutokana na idadi kubwa ya mizigo inayotarajiwa kusafirishwa kuelekea katika nchi za Congo DR, Burundi na Zambia mara baada ya kukamilika kwa reli ya kisasa ya SGR.
‘’Mkoa wa Kigoma unaendelea kufunguka na kutoa mazingira bora na wezeshi kiuwekezaji kutokana na kuimarika kwa miundombinu ya Uchukuzi na usafirishaji, ujenzi wa mfumo wa Umeme wa Gridi ya Taifa sambamba na uhakika wa upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii’’ amesema Andengenye.
Kampuni ya TAZACO Inv. Ltd imeonesha kuvutiwa nakuweka nia ya kupanua Bandari ya Kigoma ili kuongeza uwezo na kuzidi kuipaisha nchi ya Tanzania kiuchumi kupitia shughuli za kibiashara kwenye sekta ya Bandari.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa