Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Rashid Mchatta amewataka Watendaji na Maafisa wa Serikali katika wilaya za Kibondo, Kakonko, Kasulu na Buhigwe kuharakisha utekelezaji wa miradi mbalimbali na kuhakikisha miradi hoyo inakidhi Kiwango cha thamani ya fedha.
Mchatta amesema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi ya ukaguzi wa miradi inayotekelezwa chini ya Programu ya Pamoja ya Kigoma kwa ushirikiano kati ya mashirika 17 ya Umoja wa Mataifa, Sekretariati ya Mkoa na Halmashauri za Mkoa wa Kigoma. Aidha, amesisitiza na kuwaasa maafisa wa serikali na wa Umoja wa Mataifa kuzidi kuimarisha ushirikiano ili kufikia malengo ya Programu ya Pamoja ya Kigoma kwa manufaa na maendeleo ya wananchi wa Mkoa wa Kigoma kama ilivyokusudiwa na Mashirika hayo.
Katika Ziara hiyo iliyofanyika kwa siku nne kuanzia tarehe 21 hadi 24 Septemba 2020, ilihusisha kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika wilaya za Kibondo, Kakonko, Kasulu na Buhigwe. Miadi iliyotembelewa ni pamoja na Ujenzi wa Soko la Mpakani na Ghala la kuhifadhia mazao katika kijiji cha Muhangeambalo likikamilika litaimairisha biashara na ujirani mwema kati ya nchi ya Burundi na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Miradi mingine inayotekelezwa ni Dawati la Jinsia kwenye kituo cha Polisi cha Kibondo, ujenzi wa soko la mpakani la Mukarazi. Ujenzi wa Chuo cha Ufundi Malorwegwa kinachotoa mafunzo ya ufundi kwa wakimbizi na wananchi wanaoishi katika jamii jirani na Makambi ya wakimbizi, kituo cha mafunzo cha vijana ambao hawakuweza kuendelea na elimu rasmi (IPOSA) kilichopo katika shule ya msingi Busunzu kinachotoa mafunzo ya ufundi na stadi za maisha kwa vijana walio nje ya mfumo rasmi wa elimu
Vilevile katika Wilaya ya Kasulu, miradi inayotekelezwa na Mpango huu ni ujenzi wa ghala la kuhifadhi mazao unaoendelea katika Kijiji cha Mvugwe, kituo cha kuhifadhi wahanga wa ukatili dhidi ya jinsia na watoto, uboreshaji wa mradi wa maji wa Kabanga unaotekelezwa na RUWASA na.
Ziara ya ukaguzi wa miradi inayotekelezwa chini ya Programu ya Pamoja ya Kigoma, ilihitimishwa tarehe 24 Septemba 2020 kwa kutembelea maendeleo ya ujenzi wa kituo cha vijana wilaya ya Buhigwe, mradi wa ujenzi wa soko la Pamoja kwenye Kijiji cha Muyama ambako takribai vizimba 120 vitajengwa ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuinuia wanawake kiuchumi.
Katika ziara hyo Katibu Tawala aliaambatana na Maafisa mbalimbali waandamizi wa Mkoa pamoja na Halmashauri kwa kushirikiana na Mafisa wa Mashirika yanayotekeleza Programu ya Pamoja ya Kigoma.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa