KATIBU TAWALA MKOA WA KIGOMA HASSAN RUGWA AKIZUNGUMZA NA WAYTENDAJI WA IDARA YA AFYA MKOA WA KIGOMA (HAWAPO PICHANI) ALIPOKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WATENDAJI HAO KATIKA UKUMBI WA JOY IN THE HARVEST MJINI KIGOMA.
Katibu Tawala mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa amewakumbusha watendaji wa Serikali walio chini ya Idara ya Afya mkoani Kigoma kuzingatia maelekezo na maaagizo m balimbali yanayotolewa na serikali ikiwemo agizo la kutoendelea kutoza fedha kwa ajili ya kulipia kadi za Kliniki pamoja na faini kwa wanawake wanaojifungulia nje ya vituo vya kutolea Huduma za Afya.
Hayo yamejiri kufuatia katibu Tawala huyo kukutana na kuzungumza na watendaji wa Idara hiyo kwa lengo la kuwahimiza kuhusu kusimamia utekelezaji wa agizo hilo lililotolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango alipofanya ziara yake ya kikazi mkoani Kigoma na kuiagiza Wizara ya OR-TAMISEMI kuchukua hatua madhubuti ili kudhibiti suala hilo.
Ifahamike kuwa, agizo hilo lilikuja kufuatia baadhi ya wakazi katika Wilaya za Uvinza na Kasulu kutoa malalamiko kwa kiongozi huyo kuhusu kutozwa fedha katik ya Shilingi 30,000 hadi 50,000 kutokana na kujifungua nje ya kituo cha kutolea huduma za Afya sambamba na kulipia kadi za Kliniki.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt. Ibrahim Salehe amesema Idara ya Afya Mkoa wa Kigoma kwa kushirikiana na watendaji wake katika ngazi za Halmashauri imeshaanzan kutekeleza agizo hilo ikiwemo kuchapisha kadi za kutosha na kuzigawa kwa wanawake wanaojifungua kupitia vituo vyote vya kutolea huduma za Afya.
Aidha amesisitiza kuwa Ofisi ya Mganga Mkuu Mkoa haitosita kuchukua hatua dhidi ya watumishi watakaokaidi kutekeleza agizo hilo ili kuruhusu utoaji wa huduma hizo bila kuwepo kwa aina yoyote ya kikwazo.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa