Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Bw. Rashid Kassim Mchatta ambaye meapishwa hivi karibuni kushika Mkoa huo, ameahidi kushirikiana na watumishi pamoja na watendaji mbalimbali katika Mkoa wa Kigoma ili kuleta maendeleo.
Mchatta ameyasema hayo wakati wa kujitamvulisha mbele ya viongozi na watumishi mbalimbali wa Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali yaliyopo Mkoani Kigoma.
Amesema pamoja na kuwa ametoka sekta ya kifedha ambako alikuwa akifanya kazi mbalimbali za mambo ya fedha na uwekezaji, atahitaji kujifunza kwa kasi kutoka kwa watumishi na wataalam mbalimbali Mkoani Kigoma, na kuahidi kushirikiana nao ili kuleta maendeleo.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa