Mkuu wa Wilaya ya Kobondo Kanali Agrey Magwaza akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Isack Mwakisu Leo Agosti 18, 2023 katika kijiji cha Mvugwe wilayani Kasulu.
Imekuwa Siku ya kihistoria kwa kijana huyu mkazi wa kijiji cha Mvugwe wilayani Kasulu(Jina halikupatikana) ambaye tendo la kuushika Mwenge wa Uhuru litabaki kumbukumbu itakayojenga moyo wa Uzalendo daima katika Maisha yake. m
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Abdallah Kaim akifurahia Jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Joseph Kashushura (wa pili kutoka kushoto) pamoja na Mganga Mkuu wa Hospitali ya wilaya ya Kasulu Dkt. Rrobert Rwebangira (wa kwanza kushoto) mara baada ya kukagua ujenzi wa Nyumba Nne za makazi ya watumishi wa Afya.
Mbio za Mwenge wa Uhuru mkoani Kigoma zimeendelea katika wilaya ya Kasulu ambapo Leo Agosti 17, 2023 Miradi yenye Thamani ya Zaidi ya Shilingi Bil. 2 imakaguliwa kutembelewa na kuwekewa mawe ya msingi huku mmoja ukiwa ni Ugawaji wa vyombo vya usafiri kwa vijana.
Akizungumza mara baada ya Kuweka Jiwe la Msingi kwenye ujenzi wa nyuma nne za makazi ya watumishi wa Kituo cha Afya Nyakitonto, Kiongozi wa Mbio hizo za Mwenge Adballah Kaim amesema watumishi wa Umma wanapaswa kutanguliza uzalendo katika usimamizi na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa lengo ya kulinda maslahi ya Taifa.
Ili kumsauidia Rais wetu Dkt. Samia ‘’Niwaombe mzingatie maadili na nidhamu ya kazi ili kuhakikisha mnatoa huduma zenye ubora kwa lengo la kuwasaidia wananchi na kulifanya Taifa lizidi kusonga mbele’’
Katika miradi yote iliyokaguiliwa wilayani humo, nyaraka zote za matumizi ya fedha hazikuonesha uwepo wa dosari huku msisitizo ukielekezwa kwenye utekelezaji wa haraka wa maagizo yaliyotolewa na kiongozi huyo, kufuatia dosari chache za kiutendaji zilizobainika wakati wa ukaguzi wa baadhi ya miradi.
Katika wilaya ya Kasulu Mwenge wa Uhuru umezindua vyumba viwili vya madarasa Shule ya Msingi Nyamganza, kuweka jiwe la msingi katika mradi wa Maji kijiji cha Mkesha, Ujenzi wa nyumba nne za watumishi katika Hospitali ya wilaya ya Kasulu, barabara ya lami Km 0.5 pamoja na kutembelea kisha kukagua kikundi cha waendesha Pikipiki Makere na bustani ya kuzalisha miche ya miti.
Agosti 17, 2023 Mwenge huo ukiwa wilayani Kibondo, ulitembelea, kukagua na kuweka Mawe ya Msingi kwenye miradi sita yenye Thamani ya zaidi ya Shilingi Bil. 2 ambapo miradi yote ilipokelewa kisha kiongozi wa mbio hizo kutoa pongezi kwa Uongozi wa Serikali ukishirikiana na wataalam wengine katika kuhakikisha ubora na thamani ya fedha imezingatiwa katika utekelezaji wake.
PICHA MBALIMBALI ZA MIRADI NA MATUKIO KATIKA MBIO ZA MWENGE WA UHURU WILAYANI KIBONDO NA KASULU.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa