Katika kuhakikisha utekelezaji wa kupunguza vifo vya kinamama wajawazito na watoto Mkoani Kigoma; Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brig. Jen. (Mst) ameamua kukabiliana na changamoto ya uhaba wa magari kwa kuagiza magari yote ya seriakali yatoe huduma za dharula kama Magari ya “Ambulance”
Maganga ametoa agizo hilo wakati akizindua kambi ya Madaktari bingwa ambao wamewasili Mkoani Kigoma kutoa huduma ya matibabu ya magonjwa mabalimbali ya kwa muda wa siku sita katika Hospitali ya Rufaa ya Maweni.
“Wakati mwingine tunapaswa kuishi kulingana na mazingira, tuache kujifananisha nan chi zilizoendelea, gari lolote la Serikali haijalishi ni la Mkurugenzi, Mkuu wa Wilaya au Mkuu wa Mkoa kuanzia leo kama kunadharula yatumike kama magari ya dharuala ili kuokoa uhai wa wananchi” alisisitiza.
Aidha ametoa wito kwa wananchi na wadau wote Mkoani Kigoma kusaidi katika suala hili “ Ofisi yangu ipo tayari kumpatia mafuta mtu atakaye msafirisha mghonjwa kwa dharuala ili mradi tu asitutoze fedha tofauti na mafuta, niwaombe wananchi tuwe na moyo wa kizalendo kuuungana na Serikali katika kuokoa maisha ya watu wetu”.
Mkuu wa Mkoa amewashukuru Madaktari bingwa waliofika kutibu katika Hospoitali ya Rufaa ya Maweni ambapo wanategemea kuhudumia wahitaji zaidi ya watu 800. Amesema Mkuu wa Mkoa “nafarijika sana ninapoona wananchi wangu wanapata fursa za huduma za matibabu kama haya”.
Wagonjwa wengi Mkoaani Kigoma wamekuwa kipata changamoto wanapopewa rufaa ikiwemo umbali toka Mkoani Kigoma wa kuzifikia hospitali kubwa za rufaa, umaskini wa Wananchi, na ukosefu wa Madaktari. Amewahakikishia wananchi kuwa Serikali itaendeleaa kufanya jitihada kila mara ya kusogeza huduma ya tiba kwa Wananchi, ikitambua kuwa ili tuweze kuendelea na kuweza kufikia uchumi wa kati Afya za wananchi lazima ziboreshwe kwa kiwango cha juu.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa