• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko / Mrejesho |
KIGOMA   REGION
KIGOMA   REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Kigoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Seksheni ya Elimu
      • Seksheni ya Afya
      • Seksheni ya Miundombinu
      • Seksheni ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Mipango na Uratibu
      • Seksheni ya Uchumi na Uzalishaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha Fedha
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwami
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Kibondo
      • Halmashauri ya Kibondo
    • Wilaya ya Kigoma
      • Halmashauri ya Kigoma
      • Manispaa ya Kigoma Ujiji
    • Wilaya ya Kakonko
      • Halmashauri ya Kakonko
    • Wilaya ya Kasulu
      • Halmashauri ya Kasulu
      • Halmashauri ya Kasulu Mji
    • Wilaya ya Uvinza
      • Halmashauri ya Uvinza
    • Wilaya ya Buhigwe
      • Halmashauri ya Buhigwe
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Kigoma Ujiji
    • Halmashauri ya Buhigwe
    • Halmashauri ya Kasulu
    • Halmashauri ya Kasulu Mji
    • Halmashauri ya Kibondo
    • Halmashauri ya Uvinza
    • Halmashauri ya Kakonko
    • Halmashauri ya Kigoma
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Kigoma Special Economic Zone
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mikakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Picha

*KAMATI ZA MAAFA HALMASHAURI YA KIGOMA UJIJI ZAPATIWA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA MAAFA

Posted on: March 25th, 2025

Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu (Idara ya Menejimenti ya Maafa) kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia uhamaji (IOM) wameendesha semina ya kujenga uelewa juu ya upunguzaji wa madhara ya maafa katika jamii.

Mafunzo hayo yamefanyika tarehe 25 Machi 2025 katika Manispaa ya Kigoma Ujiji ambapo yamehudhuriwa na washiriki 50 ikiwemo Watendaji wa Kata, Watendaji wa Vijiji, Watendaji wa Mtaa Kamati za Maafa za Kata na Vijiji pamoja na mtaa.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Bi.Petronila Gwakila ambaye ni Afisa Mazingira ndani ya Manispaa hiyo amesema, mafunzo hayo yameletwa wakati sahihi ambapo manispaa inatarajiwa kupata mvua ambazo mara nyingi mvua hizo husababisha maafa mbalimbali na kufanya wananchi kutofanya shughuli zao za kila siku za kuwapatia kipato hivyo mafunzo haya yataweza kuleta muamko katika kukabili maafa pindi yatakapotokea.

"Kwa hiyo ndugu zangu tumepata wakufunzi hawa juu ya masuala ya Maafa ningependa sana tuwe makini kusikiliza kutokana na kwamba hili jambo ni muhimu maana si mara moja wala mara mbili maafa hasa ya mafuriko yanatukuta sana katika maeneo yetu hata sasa mvua zimeshaanza na tumeanza kuona athari zake hivyo tusikilize ili tujue namna ambavyo tunaweza kujinusuru na jambo hiliā€ alisema Bi.

Kwa Upande wake Mratibu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Idara ya Menejimenti ya Maafa Naibu Kamishina Hamisi Rutengo  amesema, lengo la kutunga Sheria ya Maafa ni kuwezesha shughuli za usimamizi wa Maafa kutekelezwa ikiwa ni pamoja na kuzingatia ushauri wa kitaalamu na maelekezo ya viongozi ili kupunguza madhara ya majanga. 

"Semina kama hizi za kujengeana uwezo zinatukumbusha namna ya kukabiliana kabla ya tukio kutokea, wakati wa tukio kutokea, na baada ya tukio kutokea kwa hiyo tupo hapa kwaajili ya kujenga uwezo huohuo wa sisi mmoja mmoja hadi ngazi ya kitaifa na serikali haikotayari kupoteza watu kwa makusudi na ndio maana tunaleta semina hizi kwenu ili mkienda huko muweze nanyi kutoa elimu kwa wengine ili tupunguze madhara mengi zaidi." alisema  Naibu Kamishana Rutengo

Nae, Afisa Miradi Msaidizi kutoka Shirika la Kimataifa linaloshughulikia uhamaji (IOM)  Bw. Reuben Mbugi amesema semina ya upunguzaji wa hatari za maafa ni moja ya shughuli za mradi wa pamoja wa Kigoma unaotekelezwa na mashirikia ya Umoja wa Mataifa lengo ikiwa ni kuhakikisha Serikali inasaidiwa katika kuweka mazingira wezeshi kwa wananchi kabla na baada ya kupata athari za Majanga mbalimbali.

Semina hii inafanyika kwa siku mbili ambapo imeanza leo tarehe 25 Machi hadi tarehe 26 Machi 2025.

Matangazo

  • MAZOEZI KWA AFYA YAKO March 23, 2017
  • UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024 September 12, 2024
  • UJIO WA MADAKTARI BINGWA MKOANI KIGOMA November 12, 2018
  • Fomu ya Usajili wa Maonesho TBS Kigoma May 01, 2022
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • DCP NARCIS MISSAMA AFANYA ZIARA MKOANI KIGOMA

    May 07, 2025
  • JAJI ASINA AKAGUA ZOEZI LA UBORESHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI-KIGOMA

    May 03, 2025
  • VYAMA VYA WAFANYAKAZI VISIGEUKE MAHAKAMA ZA KUWAHUKUMU WATUMISHI-RC ANDENGENYE

    May 01, 2025
  • PICHA; MAENDELEO YA UJENZI WA UKUMBI WA DKT. PHILIP MPANGO KATIKA OFISI YA MKUU WA MKOA WA KIGOMA

    April 30, 2025
  • Ona vyote

Video

RC ahimiza wananchi anuani za Makazi
Video nyingine

Tovuti zinazo fanana

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA BUHIGWE
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KAKONKO
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
  • HALMASHAURI YA MJI KASULU
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBONDO
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA
  • HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGOMA UJIJI
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA UVINZA

Tovuti zinazo husiana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI PORTAL
  • IKULU
  • OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    MKOA WA KIGOMA

    Anuani: S.L.P 125

    Simu: 0282802330

    Simu ya kiganjani: +255766853404

    Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://bachelorthesiswritingservice.com

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa