KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU KITAIFA ABDALLAH KAIM AKIFURAHIA JAMBO MARA BAADA YA KUZINDUA MRADI WA NYUMBA YA WATUMISHI WA AFYA KATA YA NYANSHA, HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU. KUSHOTO KWAKE NI WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, AJIRA, KAZI NA WENYE ULEMAVU PROF. JOYCE NDALICHAKO AMBAYE PIA NI MBUNGE WA JIMBO LA KASULU MJINI.
NYUMBA YA MAKAZI YA WATUMISHI ILIYOZINDULIWA LEO AGOSTI 19,2023 NA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU KITAIFA ILIYOPO KATIKA KATA YA NYANSHA HALMASHAURI YA MJI KASULU.
MATANKI YA MAJI KATIKA MRADI WA MAJI MRUSI ULIOZINDULIWA LEO AGOSTI 19, 2023 NA MBIO ZA MWENNGE WA UHURU. MRADI HUO UNAWAFIKISHIA HUDUMA YA MAJI JUMLA YA WALENGWA 5550MBIO ZA MWENGE ZIMETEMBELEA MRADI WA VIJANA ''KIKOSI KAZI IPOSA'' WENYE THAMANI YA SHILINGI MIL. 125, ULIOPO MJINI KASULU.
MRADI WA UJENZI WA MADARASA MAWILI KATIKA SHULE YA MSINGI MWIBUYE ULIOJENGWA KWA THAMANI YA SHILINGI MIL. 40. MRADI HUU UMEKAMILIKA NA UMEFUNGULIWA NA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU KITAIFA ABDALLAH KAIM.
MUONEKANO WA NDANI WA MOJAWAPO YA DARASA JIPYA KATI YA MADARASA MAWILI YALIYOFUNGULIWA NA KIONGOZI WA KATIKA SHULE YA MSINGI MWIBUYE HALMASHAURI YA MJI KASULU.
Jamii imetakiwa kuendelea kukabiliana na vitendo vya rushwa kwa kutoa taarifa kufuatia vitendo hivyo kuchangia kuzorotesha kufikiwa kwa mafanikio katika utekelezaji miradi ya Serikali.
Rai hiyo imetolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Abdallah Kaim alipozungumza na wakazi wa Mji wa Kasulu mara baada ya kuhitimisha zoezi la kuongoza mbio hizo wilayani humo.
Amesema rushwa na ubadhilifu vimeendelea kusababisha miradi mingi inayotekelezwa na Serikali kushindwa kukamilika au kukamilika bila kuwa na ubora na viwango vilivyopendekezwa na Serikali.
Katika hatua nyingine, Kaim ametoa wito kwa jamii wilayani humo kuepuka kufanya shughuli za kibinaadam katika maeneo yenye vyanzo vya Maji ikiwemo Kilimo na Ufugaji.
‘’Nasisitiza shughuli za Kilimo na ufugaji zifanyike kwa njia za kisasa hali itakayosaidia katika utunzaji Mazingira huku tukiendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika zoezi la upandaji wa miti rafiki kwa Mazingira katika maeneo yetu’’ amesisitiza Kaim.
Nae Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu) Prof. Joyce Ndalichako(Mb), amesema Serikali inaendelea kuweka kipaumbele katika miradi inayoleta ustawi endelevu na kumnufaisha kila Mtanzania.
Amesema uwekezaji mkubwa umeendelea kufanyika kwenye miradi inayohusisha Sekta za Afya, Elimu, Maji, Barabara na Umeme kwa lengo la kuwasogezea wananchi huduma hizo muhimu.
‘’Wito wangu kwenu ni kuendelea kuiunga mkono Serikali kwa kusaidia kulinda miradi yote iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na Serikali ili iweze kudumu na kutoa manufaa kwa muda mrefu zaidi’’ amesema Prof. Ndalichako.
Aidha Mwenge wa Uhuru 2023 umeridhia na kupokea Miradi minne yenye Thamani ya Shilingi Mil 714, iliyotembelewa, kuzinduliwa na kuwekewa mawe ya Msingi katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa