Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mhe. Thobias Andengenye amelipongeza Jeshi la Uhamiaji mkoani Kigoma kwa kuimarisha mifumo ya utoaji Elimu ya Uraia kwa wakazi sambamba na kuendelea kubaini na kudhibiti mianya inayotumiwa na wahamiaji haramu kuingia mkoani hapa.
Andengenye ametoa kauli hiyo alipokutana na kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji nchini. Dkt. Anna Makakala aliyepo mkoani hapa kwa ziara ya kikazi na kusisitiza kuwa pamoja na mkoa kupakana na nchi jirani katika wilaya Sita, bado jeshi hilo limeendelea kuwafikia wakazi wa maeneo ya mipakani kwa ajili ya kutoa elimu sambamba na kubaini kisha kuendelea kudhibiti mianya inayotumiwa na wahamiaji wasio na idhini za kiserikali kuingia nchini.
"Mkoa utaendelea kushirikiana na Jeshi la Uhamiaji ili kuhakikisha wanaoingia nchini kutoka nchi jirani wanazibgatia sheria pamoja na kuimarisha mifumo ya utoaji taarifa kuhusu uwepo wa raia wa kigeni katika maeneo yetu katika kwa lengo la kudumisha ufuasi wa Sheria na Usalama" amesema Andengenye.
Naye Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Nchini Dkt. Anna Makakala amesema ziara yake imelenga kuweka mikakati ya pamoja katika kuhakikisha jeshi hilo mkoani Kigoma linazidi kuimarisha mifumo ya kukabiliana na wahamiaji haramu.
"Jeshi la Uhamiaji linaendelea kushirikiana na wananchi ili kubaini vipenyo vipya ambavyo baadhi ya wahamiaji huvitumia kupita na kupitisha bidhaa kwa njia za magendo" amesema Kamishna Jenerali Makakala.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa