Jeshi la Magereza limesema limejipanga sawasawa kuanza kutekeleza maagizo Mhe.Waziri Mkuu ya kufanya Gereza la Kwitanga lililoko Mkoani Kigoma kuwa kituo kikuu cha Kilimo cha zao la Michikichi na Uzalishaji wa mafuta ya Mawese.
Haya yameelezwa na Kamisha CP Tusekile Mwaisabila wakati akizungumza na Kamati ya Ulinzi ya Mkoa wa Kigoma ambapo amefanya ziara yenye lengo la kufuatilia na kuweka mikakati mbalimbali itakayowezesha utekelezaji wa haraka wa maagizo ya Mhe. Waziri Mkuu.
Akiwa Mkoani Kigoma wakatia wa Ziara yake ya kikazi mwishoni mwa Mwezi julai aliuagiza uongozi wa gereza la Kwitanga kuongeze nguvu katika uzalishaji wa michikichi kwa kupanua mashamba na kuongeza askari wenye ujuzi wa kilimo cha michikichi na kupanda miche mipya ya michikichi na kuondoa ya zamani.
Kamishna Mwaisabila ameleza kuwa ziiara yake Mkoani Kigoma ni mahususi kwaajili ya kuja kuanza utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mku, Jeshi la Magereza limepewa jukumu la kuwa kituo kikuu cha kilimo cha michikichi na kuzalisha mafuta ya mawese “sisi kama Jeshi la Magereza tumejipanga vyema kuanza maramoja kutekeleza” amesisitiza.
Mikakati mbalimbali inayofanywa ni pamoja na kuongeza nguvu kazi ya wataalamu wa kilimo hususan wajuzi wa zao la michikichi, kutafuta fedha ya kuongeza na kuboresha mkiundombinu, pamoja na zana za kilimo cha zao la michikichi.
Amesisitiza kwamba mbali na maagizo ya Mhe. Waziri Mkuu, jeshi la magereza pia linaendelea kutekeleza maagizi ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye alilitaka jeshi hilo kuongeza kazi ya uzalishaji katika sekta mbalimbali.
Uzalishaji wa mafuta kwa miaka mitatu (3) mfululizo katika gerezani Kwitanga ulikuwa kati ya lita 12,000 hadi lita 16,000,” alisema.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa