MKUU WA MKOA WA KIGOMA THOBIAS ANDENGENYE AKIWASALIMIA WANANCHI WALIOJITOKEZA KUSHIRIKI KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKR DUNIANI KILICHOFANYIKA KIMKOA KATIKA KATA YA MAKERE WILAYANI KASULU.
MKUU WA WILAYA YA KASULU ISSACK MWAKISU(KULIA) PAMOJA MA AFISA MAENDELEO YA JAMIIMKOA WA KIGOMA MSAFIRI NZUNURI WAKIFUATILIA JAMBO WALIPOSHIRIKI KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA MWANAMKE KIMKOA.
Jamii mkoani Kigoma imetakiwa kuachana na tabia ya kumaliza mashauri yanayohusu vitendo vya ukatili wa kijinsia nje ya taratibu za kisheria na kusababisha usugu wa vitendo hivyo.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye alipozungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kimkoa yamefanyika wilayani Kasulu na kusisitiza kuwa asilimi kubwa ya matukio hayo hufanywa katika ngazi ya familia.
‘’Tafiti zinaonesha Asilimia Sitini ya matukio ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsi hufanywa na watu wa karibu au ndani ya familia huku kukiwa hakuna hatua za kisheria zinazochukuliwa hali inayosababisha matukio hayo kujirudia mara kwa mara na kuleta athari ya muda mrefu miongoni mwa wanajamii’’ amesema Mkuu huyo wa Mkoa.
Katika kufikia kasi ya mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa kundi hilo mkoani Kigoma, mkuu huyo wa mkoa amewaelekeza wakurugenzi wa halmashauri kuimarisha uratibu na usimamizi wa shughuli za kielimu na hamasa kuhusu uwekezaji na masuala ya kijinsia katika maeneo yao kwa lengo la kuleta ustawi wa jamii.
Mkuu wa Mkoa amewaelekeza watendaji hao wa Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo kuendelea kutekeleza mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, huku akiitaka jamii kutumia nafasi zao kutofumbia macho vitendo hivyo kwani athari kubwa kwa watendewa.
Andengenye amewakumbusha wanawake mkoani hapa kutumia fursa za maboresho makubwa ya miundombinu ya uchukuzi sambamba na nishati ya Umeme ili kujiimarisha kiuchumi na kujiletea maendeleo wao wenyewe, jamii zao na Taifa kwa ujumla.
‘‘Niendelelee kuwasihi wakazi katika maeneo yote ambayo miundombinu mipya imejengwa au kufanyiwa maboresho, tuendelee kuitunza ili itusaidie kwa muda mrefu kwani kutokufanya hivyo tutajikuta tunarejea kwenye adha zilizotukabili siku zilizopita’’ amesisitiza Mkuu huyo wa mkoa.
Katika kuimarisha mfumo wa Utawala bora, Mkuu wa mkoa amewakumbusha wanawake mkoani hapa, wajibu wao katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ili waweze kupata fursa ya kuonesha umahiri wao katika Ngazi mbalimbali za kiutawala.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255738192977
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa