UJENZI WA TANKI LA MAJI KATIKA KIJIJI CHA SONGAMBELE WILAYANI BUHIGWE KWA THAMANI YA SHILINGI MIL. 115 UMEZINDULIWA NA MBIO ZA MWENGE WA UHURU LEO AGOSTI 20,2023
MRADI WA UJENZI WA JENGO LA MAKAZI YA OFISI YA MKUU WA WILAYA YA BUHIGWE.KAIMU KATIBU TAWALA MIUNDOMBINU OFISI YA MKUU WA MKOA WA KIGOMA FRANCISCO MAGOTI (KUSHOTO) AKITOA UFAFANUZI KUHUSU MAENDELEO YA UJENZI WA MRADI WA JENGO LA MAKAZI YA MKUU WA WILAYA YA BUHIGWE KWA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE ABDALLAH KAIM. WA KWANZA KULIA NI MKUU WA WILAYA YA BUHIGWE KANALI MICHAEL MASALA.VIJANA WAENDESHA BODABODA KASUMO WAKIMSIKILIZA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE ADBALLAH KAIM (HAYUPO PICHANI) ALIPOTEMBELEA KIKUNDI HICHO NA KUKIZINDUA RASMIMUONEKANO WA SHAMBA LA MITI KATIKA MRADI WA HIFADHI YA MAZINGIRA, SHULE YA SEKONDARI KAHIMBA.KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU ABDALLAH KAIM AKIKAGUA KABLA YA KUWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA ZAHANATI YA KIJIJI KASUMO WILAYANI BUHIGWE.
MRADI WA UJENZI WA MADARASA MANNE KATIKA SHULE YA SEKONDARI BUHA.
ABDALLAH KAIM AMBAYE NI KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU AKIZUNGUMZA NA WANAFUNZI(SHULE HAIKUFAHAMIKA) MARA BAADA YA KUPANDA MITI KATIKA MRADI WA UHIFADHI WA MAZINGIRA KIJIJI CHA RUHEKA.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2023 Abdallah Kaim amewaelekeza Wahandisi katika Halmashauri za Mkoa wa Kigoma kujenga tabia endelevu ya kufuatilia na kutembelea mara kwa mara miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.
Kaim ametoa maelekezo hayo mara baada ya kukagua Mradi wa ujenzi wa madarasa manne katika Shule ya Sekondari Buha iliyopo wilayani Buhigwe na kusisitiza kuwa dosari ndogondogo zilizobainika katika mradi huo zimetokana na wahandisi kutokufuatilia kwa ukaribu zoezi la ujenzi wa baadhi ya miradi ya maendeleo katika maeneo wanayowajibika nayo.
‘’Hatutegemei kuona dosari ndogondogo zikiendelea kuonekana mara baada ya mradi kukamilika, hii ni ishara kuwa kuna baadhi ya wahandisi hawatekelezi ipasavyo zoezi la kukagua hatua mbalimbali za utekelezaji wa baadhi ya miradi’’ Amesema Kaim.
Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge kitaifa 2023, amesisitiza kuwa dosari zilizobainika wakati wa ukaguzi wa Miradi zifanyiwe kazi na taarifa ziwasilishwe kuendana na muda alioelekeza wa kufanyika kwa marekebisho hayo.
Aidha Kaim amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari pamoja na kujikinga na ugonjwa wa Marelia kwa kuzingatia matumizi sahihi ya vyandarua pamoja na kutumia dawa kwa ukamilifu pale wanapobainika kuwa na Maradhi hayo.
Upande wake Mratibu wa Marelia katika Halmashauri ya Buhigwe amesema Katika kipindi cha Mwaka 2022 hadi 2023 kitengo chake kimefanikiwa kutoa Elimu ya udhibiti wa marelia kwa walengwa 22,200.
Ameendelea kufafanua kuwa, changamoto ya matumizi sahihi ya vyandarua pamoja na kutozingatia usafi wa mazingira vimeendelea kusababisha kuwepo kwa ugonjwa huo katika Halmashauri ya hiyo.
Aidha Mwenge wa Uhuru wilayani Buhigwe umetembelea mradi wa Hifadhi ya Mazingira katika Shule ya Msingi Kahimba, kuweka Jiwe la Msingi Zahanati ya kijiji Kasumo, Nyumba ya Makazi ya Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe pamoja na Barabara ya Lami Buhigwe mjini.
Kadhalika Mwenge huo umezindua madarasa manne katika Shule ya Sekondari Buha, mradi wa pikipiki za kusafirisha abiria Kijiji cha Kasumo, ujenzi wa Tanki la Maji kijiji cha Songambele pamoja na kushiriki zoezi la kupanda miti katika kijiji cha Ruheka.
Miradi yote ikiwa na Thamani ya Shilingi Bil. 3.6 imepokelewa na Mwenge huo wa Uhuru
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa