Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amekabidhi pikipiki 12 na gari moja kwa watendaji wa Idara ya Afya mkoani hapa ili kurahisisha zoezi la usambazaji wa chanjo katika halmashauri za mkoa.
Akizungumza kabla ya kukabidhi vitendea kazi hivyo, mkuu huyo wa mkoa amewataka watendaji hao kuhakikisha nyenzo hizo zinatumika kama ilivyokisudiwa ili ziweze kuleta matokeo chanya kwa walengwa.
Zoezi la ugawaji wa vitendea kazi hivyo limefanyika leo Januari 28, 2025 na kushuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Rashid Chuachua ambapo amepokea nyenzo hizo akiwawakilisha wakuu wa wilaya za Mkoa wa Kigoma.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa