Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amekutana na Viongozi wa Umoja wa Madhehebu ya Kipentekoste (CPCT)Mkoa wa Kigoma na kuwataka kuendelea kuhubiri Amani na Upendo ndani ya Jamii ili kudumisha Mshikamano na kuchochea Maendeleo ya Mkoa
Kupitia kikao hicho Andengenye amesisitiza Jamii kuachana na Imani za kishirikina zinazosababisha uwepo wa matukio ya upigaji wa Ramli chonganishi (Lambalamba) na kusababisha uvunjifu wa Amani na utulivu katika baadhi ya maeneo mkoani hapa.
Aidha Andengenye ametoa wito kwa wananchi kutoa Taarifa mapema wanapobaini uwepo wa viashiria vya uvunjifu wa Amani katika maeneo yao ili Serikali iweze kuchukua hatua dhidi ya wahusika na kudumisha ufuasi wa Sheria katika Jamii.
Kwa upande wao viongozi hao wamemshukuru Mkuu huyo wa Mkoa kwa ushirikiano mzuri anaoendelea kuwapa jambo linalowapa fursa ya kuiunganisha Serikali na waumini wa madhehebu mbalimbali ya dini mkoani Kigoma.
‘’Ushirikiano unaotupa umetufanya kuwa huru kukutana na wewe a kujadili masuala mbalimbali yanayowagusa waumini wetu kama sehemu ya jamii ikiwemo kupata ushauri na hata utatuzi wa baadhi ya changamoto zinazotukabili katika maeneo tunayoyaongoza’’ wamesisitiza Viongozi hao.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa