Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Mkoani Kigoma wameagizwa kusimamia kwa nguvu zote suala la uhamasishwaji wa wananchi hususan vijana na kinamama kujiunga kwenye vikundi mbalimbali za ujasiriamali ili waweze kukopesheka katika taasisi za kifedha na mifuko mbalimbali inayotolewa na Serikali.
Akizungumza wakati wa Kikao cha wadau wa biasha kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brig. Jen. (Mst) Emmanuel Maganga amesema anataka kuona Wakuu wa Wilaya wanawasimamia ipasavyo Maafisa Maendeleo ya Jamii ili waende Vijijini kutoa elimu na kuhamasisha juu ya faid za kujiunga kwenye vikundi.
“ mimi kwanza nataka nisikie nyinyi wakuu wa Wilaya Maafisa maendele mumewaweka ndani kwani sioni wanacho kifanya, kila mahali nikifanya ziara Wilayani wananchi hawajui chochote kuhusu vikundi wala asilimia 10 inayotengwa kwaajii ya kuwakopesha kinamama, vijana na walemavu, halafu maafisa maendeleo wapo tu mnawaangalia” alisisitiza Mkuu wa Mkoa
Aidha amewaagiza wakurugenzi wote kuhakikisha fedha ya kuwakopesha vikundi asilimia 10 ya mapato ya ndani inatengwa kwa mujibu wa sheria kwani hilo ni agizo la Serikali na siyo la kupuuza, Mkurugenzi ambaye atashindwa kufanya hivyo tafsiri yake ameshindwa kazi hana msaada na wananchi wake.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa