Mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amezitaka halmashauri zote mkoani humo kupitia upya vyanzo vyake vya mapato ili kuweka utaratibu mzuri utakao saidia kuongeza mapato na kudhibiti upotevu wa fedha hiyo.
Andengenye ametoa witoa huo wakati akifungua kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa huo na kusisitiza kuwa kuna fedha nyingi zinapotea kwa sababu ya usimamizi hafifu wa baadhi ya watendaji.
Amewaagiza Wakurugenzi kushirikiana na kuziba mianya yote ya upotevu wa mapato na udhaifu mkubwa wa baadhi ya Watendaji na mifumo ya ukusanyaji isiyosimamiwa vizuri.
“Vyanzo vyetu vya mapato tunapaswa kuvipitia upya na kupanua wigo wa ukusanyaji pamoja na usimamizi thabiti katika kukusanya, bado kuna fedha nyingi zinapotea kwa sababu ya usimamizi hafifu kwa wakusanya mapato” amesema Andengenye.
Aidha amewakumbusha watendaji katika Halmashauri kuendelea kusimamia kikamilifu Suala ukusanyaji kodi, na kusimamia mifumo ya ukusanyaji kodi kwa njia ya Mashine za Kielektroniki za EFD.
Natoa msisitizo kwamba Halmashauri iimarishe usimamizi wa vyanzo vya mapato na ufuatiliaji wa makusanyo ili kufikia lengo la makusanyo ya mwaka . Kuweni wabunifu na ibueni vyanzo vipya vya mapato.Amesisitiza Mkuu wa Mkoa.
Sambamba na hayo amezitaka Halmashauri kuendelea kutenga fedha za mapato ya ndani na kuzipeleka kuchangia utekelezaji wa miradi ya Maendeleo.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa