• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko / Mrejesho |
KIGOMA   REGION
KIGOMA   REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Kigoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Seksheni ya Elimu
      • Seksheni ya Afya
      • Seksheni ya Miundombinu
      • Seksheni ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Mipango na Uratibu
      • Seksheni ya Uchumi na Uzalishaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha Fedha
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwami
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Kibondo
      • Halmashauri ya Kibondo
    • Wilaya ya Kigoma
      • Halmashauri ya Kigoma
      • Manispaa ya Kigoma Ujiji
    • Wilaya ya Kakonko
      • Halmashauri ya Kakonko
    • Wilaya ya Kasulu
      • Halmashauri ya Kasulu
      • Halmashauri ya Kasulu Mji
    • Wilaya ya Uvinza
      • Halmashauri ya Uvinza
    • Wilaya ya Buhigwe
      • Halmashauri ya Buhigwe
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Kigoma Ujiji
    • Halmashauri ya Buhigwe
    • Halmashauri ya Kasulu
    • Halmashauri ya Kasulu Mji
    • Halmashauri ya Kibondo
    • Halmashauri ya Uvinza
    • Halmashauri ya Kakonko
    • Halmashauri ya Kigoma
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Kigoma Special Economic Zone
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mikakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Picha

HALMASHAURI ZOTE KIGOMA ZAPATA HATI SAFI

Posted on: June 21st, 2023


Halmashauri Nane za Mkoa wa Kigoma zimefanikiwa kupata Hati safi za Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mujibu wa Taarifa  ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022.

Halmashauri hizo ni Manispaa ya Kigoma/Ujiji, Mji Kasulu pamoja na Halmashauri za Wilaya Kasulu, Uvinza, Buhigwe, Kibondo, Kakonko na Kigoma.

Akizungumza kwenye Mkutano wa Baraza la Maalum la Madiwani kwa ajili ya kupokea na kupitia Taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Wilayani Buhigwe, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amezipongeza Halmashauri hizo na kuzielekeza kujiwekea mikakati ya  muda mrefu itakayolenga kupunguza hoja zisizokuwa za lazima.

Amesema Taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali imebaini uwepo wa tatizo sugu la utunzaji sahihi wa nyaraka za kifedha zikiwemo zile za manunuzi pamoja na matumizi ya Masurufu.

‘’Yanapofanyika manunuzi na matumizi mengineyo ya masurufu, risiti zinazothibitisha matumizi yaliyofanyika ziwasilishwe mapema sehemu husika na aandaliwe mtu maaalum atakayeratibu na kusimamia zoezi la kuzipokea na kuzitunza ili zitakapohitajika ziweze kupatikana kwa urahisi’’ amesema.

‘’Nawaelekeza Wakurugenzi katika Halmashauri zote mkoani hapa kuanzisha Ofisi Maalum itakayotekeleza jukumu la utunzaji wa Nyaraka za Manunuzi katika Miradi inayotekelezwa na Serikali kwenye Halmashauri hizo. Tukifanaya hivyo itatusaidia kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa nyaraka muhimu kwa ajili ya kujibu hoja za ukaguzi’’ amesisitiza Andengenye.

Ameendelea kusema, Kitengo cha Manunuzi na Ugavi kimeendelea kuwa kinara kwenye kuzalisha hoja za ukaguzi ambapo amewataka wakuu wa vitengo hivyo kuhakikisha utendaji wao unazingatia Sheria na Kanuni za Manunuzi ili kuepuka kusababisha hoja ambazo kimsingi zinaweza kuzuilika.

Aidha Mkuu wa Mkoa amezitaka Menejimenti katika Halmashauri zote za Mkoa wa Kigoma kuibua vyanzo vipya vya Mapato, kuimarisha vile vinavyoonekana kusuasua, kufuatilia utendaji kazi wa wakusanya mapato pamoja na mashine za kukusanyia mapato hayo.

‘’Nasisitiza fuatilieni na kubaini changamoto zilizopo kwenye zoezi zima la ukusanyaji wa mapato, mtakapobaini  mashine zenye dosari ziondoeni kwenye mfumo na watendaji watakaobainika kufanya ubadhirifu wa Fedha za Makusanyo wachukuliwe hatua za kisheria’’ amesisitiza Mkuu wa Mkoa.

Upande wake Mkaguzi Mkuu wa Nje wa Hesabu za Serikali CPA Honest Muya amesema pamoja na kupatikana kwa Hati hizo Safi kwa Halmashauri za Mkoa wa Kigoma, Menejimenti zinatakiwa kutoa ushirkiano mkubwa kwa wakaguzi wa ndani.

‘’Hoja huanza kuibuliwa na wakaguzi waliopo katika ngazi za Halmashauri na zinapokosa utatuzi, ndipo hufika ngazi ya mkaguzi wa nje, hivyo wakaguzi wa ndani wakipewa ushirikiano wa kutosha hoja nyingi zitaishia katika ngazi ya Halmashauri’’ ameshauri Muya. 

Kuhusu kukabiliana na hoja za zamani, Muya amesema ni muhimu kila  Halmashauri kuweka mikakati ya muda mrefu na yenye kuleta matokeo chanya ili kuhakikisha hoja hizo zinapunguzwa au kufutwa kabisa.




Matangazo

  • MAZOEZI KWA AFYA YAKO March 23, 2017
  • UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024 September 12, 2024
  • UJIO WA MADAKTARI BINGWA MKOANI KIGOMA November 12, 2018
  • Fomu ya Usajili wa Maonesho TBS Kigoma May 01, 2022
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • DCP NARCIS MISSAMA AFANYA ZIARA MKOANI KIGOMA

    May 07, 2025
  • JAJI ASINA AKAGUA ZOEZI LA UBORESHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI-KIGOMA

    May 03, 2025
  • VYAMA VYA WAFANYAKAZI VISIGEUKE MAHAKAMA ZA KUWAHUKUMU WATUMISHI-RC ANDENGENYE

    May 01, 2025
  • PICHA; MAENDELEO YA UJENZI WA UKUMBI WA DKT. PHILIP MPANGO KATIKA OFISI YA MKUU WA MKOA WA KIGOMA

    April 30, 2025
  • Ona vyote

Video

RC ahimiza wananchi anuani za Makazi
Video nyingine

Tovuti zinazo fanana

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA BUHIGWE
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KAKONKO
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
  • HALMASHAURI YA MJI KASULU
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBONDO
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA
  • HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGOMA UJIJI
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA UVINZA

Tovuti zinazo husiana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI PORTAL
  • IKULU
  • OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    MKOA WA KIGOMA

    Anuani: S.L.P 125

    Simu: 0282802330

    Simu ya kiganjani: +255766853404

    Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://bachelorthesiswritingservice.com

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa