Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye amezitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa mkoani humo kuhakikisha zinaweka msukumo na dhamira ya dhati katika eneo uwezeshaji wa makundi maalum kwa kutenga na kutoa mikopo kupitia asilimia 10 (kumi) kwa makundi ya kina mama, Vijana, Wenye Ulemavu ili kusaidia watu kukuza na kupa mitaji.
Andengenye amesema hayao wakati akifungua Kikao cha Ushauri cha Mkoa. Ameongeza kuwa agizo la Serikali la kuwawezesha makundi ya kina mama, Vijana, na Wenye ulemavu kupitia asilimia 10 (kumi) ya makusanyo ya ndani ya Halamsahauri linalenga kutoa mitaji kwa makundi hayo ili kutengeneza ajira na kukuza uchumi.
“Hakikisheni mnatekeleza, maagizo haya kwani ni ya msingi kwa maendeleo ya watu wetu. Kuna vijana na Wananchi wenye ari ya kukuza uchumi na pengine kutengeneza ajira lakini wanakosa fursa kwa kukosa mitaji” alisema Mkuu wa Mkoa.
Ameongeza kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa ziangalieni namna ya kukopesha makundi hayo na hata kwa mtu mmoja mmoja kwa kumpima uwezo wake wa marejesho kuliko kuangalia mtu makundi peke yake ili kutengeneza ajira nyingi kwa wananchi, napengine kupitia uwezeshaji wa makundi haya Halmashauri pia itapanua wigo wa ukusanyaji mapato.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa Andengenye ameziagiza Halmashauri kuhakikisha maeneo yote yaliyotengwa kwa ajili ya viwanda, Uwekezaji na Machinga Mkoani Kigoma kuwa na miundombinu wezeshi ili kurahisisha kila sekta kufanya kazi bila usumbufu.
Amesema katika hali isiyokuwa ya kawaida Mamlaka za Seriakali za Mitaa zimeishia zimebainisha na kutenga maeneo tu bila kuwepo na huduma na miundombinu muhimu ambayo inapaswa kuwepo ili kutoa huduma kwa watumiaji kama vile umeme, maji, barabara na huduma nyinge kulingana na shughuli zilizopo kwenye maeneo husika.
Amesisitiza kupitia vikao vya Mabaraza viangalie na namna ya kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha maeneo yanayotengwa yanakuwa na miundombinu stahiki.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa