Halmashauri za Mkoa wa Kigoma zimepewa muda wa mwaka mmoja kuanza ujenzi wa mabanda ya Maonesho yenye hadhi ya Kimaonesho kwaajili ya maonesho ya Nanenane ili kuwa na tija ya maonesho hayo kwa wakulima.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brig. Jen. (Mst) Emanuel Maganga ambaye alikuwa Mgeni rasmi wakati wa kufunga maonesho ya Nanenane kanda ya Magharibi yaliyofanyika Mkoani Tabora.
Mhe. Maganga amesema, hajaridhishwa na mabanda ya maonesho ya Halmashauri za Mkoa wa Kigoma ambao pamoja na kugawiwa viwanja ili wajenge mabanda ya maonesho bado zimekuwa zikisuasua matokeo yake hazioneshi ufanisi mzuri katika kutoa fursa kwa Wakulima wa Mkoa wa Kigoma kuonesha bidhaa zaonkatika maonesho ya Nanenane.
Uanzia leo nataka muende mwendo wa kasi hadi kufikia maonesho ya nanenane mwaka 2019 nataka nione Halmashauri za Mkoa wa Kigoma zote ziwe na mabanda mazuri yenye hadhi ya maonesho, haiwezekani kila mwaka ushiriki wa Halmashauri za Kigoma zinakuwa legelege katika hili, ameongez Mhe. Maganga.
Awali akimkaribisha mgenibrasmi mwenyeji wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwanri alisema sherehe za nanenane ni mahususi kwa waklima kubadilishana na kujifunza mambo mbalimbali namna ya kuongeza tija katika uzalishaji wa Kilimo kwa lengo la kukuza sekta ya Viwanda ambayo ni lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga nchi ya Viwanda.
Kaulimbiu ya maonesho ya Sherehe za Wakulima nanenane nchini Mwaka huu ilikuwa "wekeza katika kilimo na Uvuvi kwa maendeleo ya Viwanda" kwa upande wa kanda ya mgharibi maonesho ya naenane yamehusisha mikoa ya Tabora na Kigoma.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa