Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameuagiza Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza kukamilisha jengo na miundombinu ya kuhifadhia samaki katika Mwalo wa Muyobozi uliopo kitongoji cha Muyobozi Kijiji cha Mwakizega ili uanze kufanya kazi kwa manufaa ya wananchi na kuingizia mapato Serikali.
Makamu wa Rais ametoa maagizo haya wakati wa ziara Mkoani Kigoma alipokagua maendeleo ya mradi huo Mradi wa mwalo wa Muyobosi ambao upo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira ulianza kujengwa tangu mwaka 2013 hadi sasa umegharimu kiasi cha Shilingi milioni 482 bado unakabiliwa na ukamilishwaji wa miundombinu mbalimbali kama vile umeme, maji, pamoja na uwepo wa taasisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania, Uhamiaji.
Akisoma taarifa ya mmradi huo Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza, Mhandisi Weja Ngolo amesema kunahaja kupbwa ya kupatiwa kituo cha forodha katika Mwalo wa Muyobozi ili kukusanya mapato na kudhibiti utoroshwaji wa bidhaa mbalimbali kwenda nje ya nchi hususan Congo DRC na Burundi.
Ameongeza kuwa eneo kubwa la mwambao wa Ziwa Tanganyika Wilayani Uvinza halina kituo cha forodha hivyo mazao mengi kama vile madini ya chokaa na misitu yamekuwa yakitorishwa kupitia bandari bubu zilizopo katika mwambao huo; hivyo kuifanya Halmashauri na Serikali kwa ujumla kukosa mapato ambayo yangetokana na ushuru. Aidha ameeleza kuwa uwepo wa kituo cha forodha na taassis nyingine kama Uhamiaji katika Mwalo huo utasaidi kudhibiti uhamiaji haramu.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mhe. Mwanamvua Mirindoko amemueleza Mhe. Makamu wa Rais kuwa kwa sasa mwalo wa Muyowosi unauwezo wa kuhudumia wavuvi 1200 kwa siku na huweza kupokea tani 70 hadi 80, hadi kufikia mwaka 2018 makusanyo yameongezeka kutoka Shilingi milioni 28.3 kutoka Shilingi milioni, 3 mwka 2016. Hivyo kuwekwa rasmi kwa mwalo huo utaleta manufaa kwa wananchi Wilayani Uvinza na Serikali kwa kuwaletea maendeleo na kukuza uchumi.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa