HALAMSHAURI ZA SISITIZWA SUALA LA MOTISHA KWA WAFANYAKAZI
Posted on: October 30th, 2017
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Charles Pallangyo amefungua warsha ya siku sita yenye lengo la kuzijengea uwezo Halmashauri za Mkoa wa Kigoma kuandaa mpango kazi wenye lengo la kutoa motisha na vivutio kwa watumishi ili waweze kubaki katika maeneo ya vituo vya kazi wanapopangiwa.
Amesema maeneo yaliyopo pembezoni ambako huduma za kijamii, kiuchumi na miundombinu bado havijaimarika na hivyo kuwa changamoto kwa watumishi wanapopangiwa kazi katika maeneo hayo.
Akiwashukuru wafadhili wa mafunzo hayo Shirika la Marekani USAID kupitia PS3, amesema warsha hiyo itasaidia serikali za mitaa kuwa na uwezo sio tu wa kuwabakisha watumishi wanapopangiwa kufanya kazi bali pia kuinua kiwango cha ubora wa huduma zinazotolewa kwa wananchi.
“Nataka niwaeleze viongozi wa halmashauri mnapaswa kusimamia zoezi hili ili liwe endelevu tukifanya kazi yetu vizuri, wafanyakazi ari ya kufanya kazi pia kupunguza idadi ya wafanyakazi kutokaa maeneo ya kazi pindi wanapopangiwa alisema” Pallangyo.
Naye Afisa Sera na uraghabishi wa shirika la PS3 Christina Godfrey, amsema wameamua kutoa mafunzo haya baada ya kufanya utafiti kwa halmashauri 33 nchini Tanzania ambapo katika maeneo yenye changamoto Kigoma nayo ilionekana kuwa miongoni. PS3 imeona kuna umuhimu wa kutengeneza mazingira rafiki ya kikazi kwa kuwafundisha watendaji katika Halmashauri kuwa na mipango mkakati ya kutoa motisha kwa wafanyakazi.
Warsha hiyo imehudhuriwa na Maafisa Utumishi, Maafisa Elimu na Makatibu wa Hospitali kutoka katika Halmashauri za Mkoa wa Kigoma.